January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi watetewa bungeni

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereila Ame Silima

Spread the love

SERIKALI imesema, nyumba za askari polisi na magereza zilizopo eneo la Nshambya na Miembeni katika Manispaa ya Bukoba ni za siku nyingi na zimechakaa. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereila Ame Silima alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Conchester Rwamlaza (Chadema).

Rwamlaza alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwapatia askari polisi na magereza makazi bora.

“Nyumba za askari wa polisi na magereza zilizopo katika eneo la Nshambya na Miembeni katika Manispaa ya Bukoba ni za miaka mingi na zimechoka sana, je serikali ina mpango gani wa kuwapatia askari hao makazi bora?” alihoji Rwamlaza.

Akijibu swali hilo Silima amesema, ni kweli nyumba hizo simechakaa kutokana na kuwa nyumba hizo ni za siku nyingi.

“Mahitaji ya nyumba za askari ni makubwa ambapo uwezo wa askari kufanikisha ujenzi wa nyumba hizo kwa wakati mmoja ni mdogo.

“Ili kupambana na tatizo hilo jeshi la magereza limepanga kulifanyia ukarabati jengo la ghorofa nne linalokaliwa na familia 72 lililopo kata ya Miembeni katika Manispaa ya Bukoba,” amesema Silima.

Amesema ukaratabi huo utahusisha kupaka rangi, mfumo wa maji taka, maji safi na umeme na ukarabati huo utafanyika katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16 endapo serikali italipatia jeshi fedha hizo.

Akiendelea kujibu maswali hayo amesema kutokana na uchakavu mkubwa wa nyumba za jeshi la polisi eneo la Nshambya serikali haina mpango wa kukarabati nyumba hizo.

Amesema nguvu nyingi itaelekezwa ukamilishwaji wa ujenzi wa ghorofa tatu lenye uwezo wa kuchukua familia 36 eneo la Buyekera.

“Serikali iko mbioni kujenga maghorofa mawili yenye uwezo wa kuchukua familia 24 eneo la Nshambya ilipo Kambi ya FFU Bukoba Mjini,” amesema.

error: Content is protected !!