ABDURAHMAN Kaniki, Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ameshauri askari wanaoanza kazi kujiunga na Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Usalama wa Raia (URA- Saccos) kwani jeshi hilo lina mpango wa kutoa mkopo wa Sh. 2,000,000 kwa kila mwanachama mpya, anaandika Christina Raphael.
Inspekta huyo amesema hayo leo wakati wa kikao cha mkutano mkuu wa saba wa Saccos hiyo uliofanyika mjini hapa.
Amesema kuwa, wanachama wapya hukopeshwa fedha hizo ili waweze kujikimu wakati wanaanza maisha baada ya kutoka chuoni, mkopo ambao hulipwa kidogo kidogo.
Amewaagiza viongozi wa Saccos hiyo kuweka utaratibu wa kupata wanachama wapya wanaotoka chuoni (depo) ili kuweza kuiboresha pia kuboresha maslahi ya polisi.
Akizungumza kwenye kikao hicho Thobias Andengenye, Mwenyekiti wa URA Saccos ambaye pia ni Kamishana wa Utawala na Rasilimaliwatu Jeshi la Polisi mesema, lengo lao ni kuhakikisha askari wa chini wanapata fursa ya kujiunga ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Amesema kuwa askari wanayo fursa kubwa ya kuitumia saccos hiyo kwa ajili ya manufaa yao kwani watawezakukopeshwa kutokana na fedha watakazokatwa kwenye mishahara yao.
More Stories
NMB yaahidi kuendelea kutoa mikopo wawekezaji nishati nchini
TARI yaongeza mnyororo wa thamani wa korosho
RPC Muliro: Marufuku mashabiki kwenda na silaha kwa Mkapa