Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu wawili, kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya Barke Pesa Rashid (30), kwenye nyumba ya kulala wageni ‘Guest House’ iitwayo Maridadi, iliyoko Tabata, jijini humo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 25 Januari 2022 na Kamanda wa Jeshi la Polisi la kanda hiyo, ACP Jumanne Muliro.

Kamanda Muliro amesema watuhumiwa hao ambao ni Kassim Said Abdallah maarufu kama Jonsiner Bounser (34) na mwingine Charles Greogory White (31), walikamatwa tarehe 23 Januari mwaka huu.

Wanadaiwa kutekeleza tukio hilo tarehe 1 Januari 2022, kwa kumkaba shingo Barke hadi kupoteza maisha.

Kamanda Muliro amesema kuwa, chanzo cha mauaji hayo, ni White kumpa kazi Baunsa ya kufanya mauaji hayo, kwa madai kuwa alimhudumia marehemu Barke ikiwemo kumpangishia nyumba, lakini mwanamke huyo alikuwa na wanaume wengine.

“Inadaiwa mtuhumiwa wa kwanza alikodiwa na mtuhumiwa wa pili White, kwa malipo ya Sh. 1.7 milioni ili amtongoze na baadae aende kumuua mwanamke huyo, kwa madai kuwa mtuhumiwa wa pili alimgharamia sana na kumpangishia nyumba, lakini ilidaiwa na mtuhumiwa wa pili kuwa mwanamke huyo ana wanaume wengine,” amesema Kamanda Muliro.

Kamanda Muliro amesema “baada ya mahojiano ya kina baunsa alikiri kufanya mauaji yale ya kinyama huku akidai alikodishwa na mwenzake wa pili Greogory kwa malipo ya pesa Sh. 1.7 milioni na kwamba alipewa Sh. 1.2 milioni na alikuwa anadai 500,000.”

Amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani ili hatua za kisheria zichukuliwe.

2 Responses

  1. Kwaiyo mapenzi mkabe mtu na kumtowa Figo acheni kutuchangamya. Tunaomba atajwe mtu aliyemtowa figo inaonyesha Ni doctor mzuri na mtueleze vizuri au kisa magufuri hayupo

  2. Kwaiyo mapenzi mkabe mtu na kumtowa Figo acheni kutuchangamya. Tunaomba atajwe mtu aliyemtowa figo inaonyesha Ni doctor mzuri na mtueleze vizuri au kisa magufuri hayupo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *