July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wasaliti kuadhibiwa vikali

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa, itawachukulia hatua kali askari wote ambao hawafanyi kazi zao kwa uaminifu hususan katika kushughulikia uthibiti wa madawa ya kulevya. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa Bungeni na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Walemavu, Dk. Abdallah Possi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantumu Dau Haji (CCM).

Katika swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua serikali inawachukulia hatua gani baadhi ya askari ambao wamekuwa wakiwafumbia macho baadhi ya watu ambao wanafanya biashara ya dawa za kulevya.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo, alitaka kujua serikali imejipanga vipi kuwanusuru wanaotumia dawa za kulevya ukizingatia vijana hao ni nguvu kazi ya taifa.

Akijibu maswali hao Dk. Possi amesema kwamba serikali inatambua matumizi ya dawa za kulevya kuwa yanasababisha madhara makubwa kwa watumiaji.

Amesema kwa kutambua tatizo hilo, serikali imechukua hatua mbalimbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza juhudi za dhati na za kimkakati kuhakikisha wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wanakamatwa na kuadhibiwa vikali kupitia sheria Na.5 ya 2015.

Amesema serikali imeendeleza huduma njema na endelevu ya kutoa matibabu kwa watumiaji wa dawa za kulevya katika hospitali na vituo vya magonjwa ya akili ili kuwasaidia watumiaji wa dawa hizo wanaacha.

error: Content is protected !!