March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi ‘wapora’ simu ya Zitto Kabwe

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo

Spread the love

JESHI la Polisi limeishikilia simu ya mkononi ya Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na muda huu wanatarajia kwenda makao makuu ya chama hicho kwa ajili ya upekuzi, anaandika Faki Sosi.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma mjini amefika kituo cha polisi kinachohusika na akosa ya fedha kilichopo jijini Dar es Salaam mahojiano kama alivyotakiwa alivyokamatwa Oktoba 31 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama hicho, Ado Shaibu imeeleza kuwa kiongozi huyo leo baada ya kumaliza mahojiano alichukuliwa simu yake.

Hata hivyo, jeshi hilo limetoa taarifa kuwa litakwenda ofisi za chama hicho kwa ajili ya kwenda kufanya upekuzi kutafuta nyaraka mbalimbali wanazohitaji.

Zitto ameechiwa kituoni hapo majira ya saa tano asubuhi na kutakiwa arudi tena kurudi Novemva 21 mwaka huu.

error: Content is protected !!