Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wapigwa msasa kesi za ukatili wa kijinsia, haki za binadamu
Habari Mchanganyiko

Polisi wapigwa msasa kesi za ukatili wa kijinsia, haki za binadamu

Spread the love

 

BAADHI ya maafisa wa Jeshi la Polisi na waendesha mashtaka, kutoka mikoa ya Kanda ya Kusini, wamepewa mafunzo juu ya namna ya kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia, watoto na haki za binadamu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Shirika la Door of Hope, yamefanyika leo Jumatatu, tarehe 25 Julai 2022, mkoani Mtwara, ambapo yamehusisha maafisa wa polisi na waendesha mashtaka kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema wameandaa mafunzo hayo ili kuwaongezea morali Polisi, waendesha mashtaka na wadau wengine katika mikoa hiyo, kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan, katika jukumu lake la kikatiba la utetezi wa haki za binadamu.

“Tunafanya kazi hii kwa ajili ya kumsaidia Rais na tulimwambia wewe ni mtetezi wa haki za binadamu namba moja Tanzania. Hivyo Rais hawezi kuifanya kazi hii peke yake na kwamba sisi sote ni watetezi wa haki za binadamu na tunafanya kazi pamoja,” amesema Olengurumwa.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Doo of Hope, Clemency Mwombeki, amesema wameandaa mafunzo hayo wakiamini kwambba Askari Polisi ni wadau muhimu wanaoshughulikia watuhumiwa wa makosa ya ukatili wa kijinsia na haki za binadamu.

“Tunaamini Jeshi la Polisi ndiyo wafau muhimu sababu wanaoshikwa wanakuja mikononi mwenu. Tuna nafasi ya kuunganisha nguvu na asasi za kiraia, waandishi wa habari kuhakikisha tunakabiliana na vitendo hivi kwenye maeneo yetu,” amesema Mwombeki.

Akiwakilisha maafisa Polisi waliohudhuria mafunzo hayo, Afisa wa Polisi kutoka katika Dawati la Jinsia mkoani Mtwara, Inspekta Adelina Nyamukama, amesema wameshiriki ili wajifunze kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia pamoja na kujua hali ya haki za binadamu katika mikoa ya Kusini.

Inspekta Nyamukama amesema, matukio ya ukatili wa kijinsia katika mikoa hiyo yamepungua kwa asilimia 11.3, kutoka 1,320 mwaka 2021 hadi kufikia 914.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!