January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wapewa elimu ya sheria ya mitandao

Spread the love

SERIKALI imeanza kutoa elimu kwa Jeshi la Polisi kuhusu Sheria mpya ya makosa ya mitandao na miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015. Anaandika Faki Sosi, DSJ … (endelea).

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa amesema kuna umuhimu wa Jeshi la Polisi kuwa na uelewa wa sheria hiyo ya mtandao.

Amesema kuwa sheria hiyo ambayo ilipitishwa bungeni 11 Aprili, 2015 ili kudhibiti uhalifu wa mtandaoni ambao umeongezeka na kukua kwa kasi kutokana na maandeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama).

“Tumeanza kutoa elimu kwa polisi kuanzia leo, mpaka sheria hiyo itakapoanza kutumika rasmi, Septemba mosi kwama huu,” anasema Prof. Mbarawa.

Prof, Mbarawa amesema kuwa wizara ya hiyo imejipanga kutoa elimu hiyo kwa polisi kutokana kuwa wao ndio wadau wakubwa wa utekelezaji wa sheria.

Aidha amesema kuwa kukuwa kwa teknolojia hiyo ya Tehama imeleta maandeleo nchini ya kuharakisha na kuboresha huduma kwa wananchi na kukuza uchumi.

Sheria hiyo ya mtandao itaanza kutumika rasmi Septemba mosi, mwaka huu.

error: Content is protected !!