Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi wapeleka majonzi Chadema
Habari za Siasa

Polisi wapeleka majonzi Chadema

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Morogoro limewasaka, kuwanasa na kisha kuwapandisha kizimbani wabunge wawili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Mwandishi Wetu Morogoro…(endelea).  

Wabunge hao Peter Lijuakali, Mbunge wa Kilombero na Susan Kiwanga, Mbunge wa Jimbo la Mlimba yote ya mkoani humo wamepandishwa kizimbani leo tarehe 25 Februari 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

Wamefikishwa mahakamani hapo ikiwa ni baada ya kusota rumande kwa zaidi ya siku tano tangu walipokamatwa na jeshi hilo.

Awali, jeshi hilo lilitoa maelezo kuwa, linawasaka ili kuwafungulia mashtaka kwa tuhuma za kufanya uhalifu kwa kuchoma moto Shule ya Sekondari ya Kijiji cha Sosi, wilayani Malinyi.

Tarehe 20 Februari 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema jeshi hilo limejipanga kwa kuwa na ushidi na vielelezo vya kutosha vya kuwatia hatiani.

Hata hivyo, kwenye tuhuma hizo mahakama hiyo iliwaacha huru wabunge hao pamoja na wanachama 13 wa chama hicho waliokuwa wakituhumiwa kutenda uhalifu huo kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yao.

Hata hivyo, siku chache baada ya kuachwa huru, jeshi hilo lilianza kukamata upya wanachama hao ambapo saba kati ya 13 walikuwa tayari wametiwa nguvuni.

Hayo yakiendelea wakati ambao chama hicho kinaendelea kuuguliwa maumivu kutokana na mwenyikiti wake Taifa-Freeman Mbowe na Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini kuendelea kusota mahabusu kwa kunyimwa dhamana.

Katika kesi yao ya msingi, Mbowe Matiko na wengine saba wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018 maeneo ya Dar es Salaam.

Wengine ni Mbunge wa Peter Msigwa, Iringa mjini; John Mnyika, Mbunge wa Kibamba na Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji.

Pia wamo Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda; Mbunge wa Kawe, Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

error: Content is protected !!