January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wang’ang’ania vifaa vya LHRC

Spread the love

JESHI la Molisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeendelea kupiga danadana kesi inayoikabili Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilichopo Mbezi Beach. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Jeshi la Polisi lilivamia katika kituo hicho Oktoba 29, mwaka huu na kupora kompyuta za mezani 24, kompyuta mpakato tatu, simu za ofisini 25 pamoja na simu binafsi za watumishi wa ofisi hiyo, kwa madai kituo hicho kilivunja sheria za mitandaoni ya mwaka 2015 kifungu cha 16 kwa kukusanya na kusambaza taarifa mitandaoni kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa kituo cha polisi cha kati Mkurugenzi wa uwezeshaji na uwajibikaji LHCR, Imerda Urio amesema, polisi walivamia kituoni hapo mida ya saa 8 mchana na kuondoka na watumishi 36 wa kituo hicho saa 12 jioni. baadae waliachiwa kwa dhamana.

“Leo ni mara ya nne tunazungushwa hapa polisi, na wamesema hawataturudishia vifaa vyetu hadi uchunguzi wao utakapokamilika, sasa kuna baadhi ya watumishi ambao walikuja kwa kazi maalumu kama wachunguzi wa uchaguzi wa ndani ambao wameshaondoka na simu zao zilichukuliwa siku hiyo hivyo hatuna mawasiliano nao, tunaomba Jeshi la Polisi litende haki kwani hasi leo hatufanyi kazi,” anasema Urio.

Aidha Urio ametoa rai kwa viongozi wa juu na mashirika binafsi kuingilia kati suala hilo kwa kile alichoeleza kuwa kituo hicho hakikukiuka sheria za mitandaoni na kwamba, walipata kibali kutoka Tume Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Wakati huohuo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ametolea ufafanuzi kesi hiyo na kudai kuwa, kabla ya polisi kuvamia kituo hicho, zilipatikana taarifa za kuaminika kuwa kutuo hicho kinafanya kazi nje ya mipaka yake na kuingilia kazi za NEC.

Kova ameongeza, kituo hicho kilikiuka makubaliano yaliyotolewa na NEC ambapo hawakutakiwa kutoa taarifa yoyote ya matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika kabla ya kupeleka matokeo hayo NEC, hivyo kituo hicho kilivunja makubaliano licha ya kupewa kibali cha kukusanya taarifa kama wakaguzi wa ndani.

Amesema, baada ya vifaa hivyo kukamatwa, vilikaguliwa na kitengo maalumu cha polisi kinachohusika na makosa ya mitandaoni na kubaini kuwa kituo hicho kilifanya kazi kwa makosa na kukiuka katiba ya NEC ya mwaka 2005.

“Kazi iliyokuwa ikifanywa na LHCR ingeweza kupelekea uvunjifu wa amani nchini kwa kusambaza matokeo yasiyo rasmi ndio maana bado tunavishikilia vifaa hivyo hado uchunguzi utakapokamilika, hakuna mtu atakauyeonewa wala kupigwa sheria itafata mkondo wake,” amesema Kova.

Kova amesema kesi hiyo itapeleka kwa mwanasheria mkuu wa serikali wiki ijayo na kila mmoja atahukumiwa kwa kosa lake.

error: Content is protected !!