October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wanasa mtandao wizi wa magari ya umma

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu 15 wanaodaiwa kujihusisha na mtandao wa wizi wa magari,ikiwemo magari ya umma. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 6 Novemba 2018, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Liberatus Sabas amesema katika operesheni iliyofanywa na jeshi hilo, wamefanikiwa kukamata magari saba ikiwemo gari la wizara ya afya na la taasisi ya wanawake Tanzania.

Amesema katika watuhumiwa 15, mmoja wao aliyefahamika kwa jina la Dk. Yusuf Mwaipopo (42) alikamatwa na gari ya wizara ya afya.

“Natoa rai kwa madereva wa magari ya umma kwamba sehemu sahihi ya kupaki magari sio kwenye yadi za uchochoroni, magari ya umma yapaki kwenye ofisi za umma zenye ulinzi wa kutosha,” amesema Kamanda Sabas.

error: Content is protected !!