August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi: wanaoporwa mamilioni hawatunzi siri

ACP Advera Bulimba Senso, Msemaji wa Jeshi la Polisi

Spread the love

WASAFIRISHAJI wa fedha wametakiwa kuwa na usiri katika michakato yote inayohusiana na usafirishaji wa fedha ili kuepuka matukio ya kuvamiwa na majambazi, anaandika Pendo Omary.

Mbali na kuwa na usiri, pia wafanyabiashara hao wametakiwa kuepuka kubeba kiasi kikubwa cha fedha na badala yake watumie miamala ya kibenki ili  kupunguza uwezekano wa kuvamiwa na kuuibiwa.

Rai hiyo imetolewa leo na ACP Advera Bulimba Senso, Msemaji wa Jeshi la Polisi katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Uchunguzi waJeshi la Polisi umebaini kuwa uhalifu umekuwa ukisababishwa wafanyabiashara husika kutokuwa na usiri na kutokuomba ulinzi wa polisi au hata makampuni binafsi ya ulinzi yanayoshughulika na kusafirisha fedha,” amesema ACP Senso.

Pia Jeshi la Polisi limewakumbusha wananchi kuwa makini wanapofanya biashara kwa njia ya mtandao wa intaneti kwani wengi wamekuwa wakiripoti kutapeliwa kutokana na tamaa za mafanikio ya haraka au kutokuwa na uelewa wa baiashara husika.

error: Content is protected !!