January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wamwekea ngumu Lowassa

Spread the love

JESHI la Polisi Makao Makuu limepiga marufuku maandamano au mikutano ya hadhara yoyote kufanyika katika kipindi hiki. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuandika barua Kanda maalum ya Dar es Salaam ya kutoa taarifa ya kutaka kufanya mikutano ya hadhara kwa nchi nzima.

Barua hiyo iliyoandikwa na Chadema Novemba 6, mwaka huu, ikieleza kuwa chama hicho kinatarajia kufanya mkutano wa hadhara siku ya Jumapili katika uwanja wa Jagwani na kwamba, Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe na Mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa ndio walitarajiwa kuhutubia mkutano huo. Baada ya kupata barua hiyo Bulimba amesema kuwa, tathmini iliyofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini inaonyesha kuwa, bado kuna mihemko ya kisiasa ndani ya jamii.hivyo maandamano ya aina hiyo inaweza kusababisha machafuko nchini.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Advera Bulimba amesema, Jeshi la Polisi bado linasisitiza katazo lake la awali lililozuia mikutano na maandamano ya aina yoyote mpaka pale hali itakapotengemaa.

“Kuna baadhi ya vyama hapa nchini vimeomba kufanya mikutano ya hadhara na maandamano yasiyo na kikomo hivyo hali hiyo inatutisha ndio maana tunazuia ili kuhakikisha usalama wa raia,” amesema Bulimba.

Bulimba ametoa wito kwa wananchi wote kutojihusisha na vitendo vyovyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani nchini na badala yake waendelea na shughuli za ujenzi wa taifa.

Afisa Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene ili kutolea ufafanuzi suala hilo simu yake iliita bila kupokelewa.

error: Content is protected !!