September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wamvaa Mbatia, aitwa kujieleza

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi

Spread the love

ZIARA ya James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi imeingia shubiri mkoani Mbeya baada ya polisi kuvamia na kuzuia mkutano wake wa ndani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

“Kwasasa naomba nisiseme chochote mpaka niitikie wito,” ameeleza Mbatia alipouliza kuhusu sababu za kuzuiliwa kufanya mkutano wake wa chama leo tarehe 5 Machi 2020.

Taarifa zaidi zinadai, Mbatia ameanza ziara kwenye eneo hilo kinyume na agizo la Rais John Magufuli, kwamba wabunge na madiwani wafanye siasa katika ameneo yao.

“Nikifika polisi na kuzungumza nao, ndio nitakuwa na nafasi nzuri ya kueleza,” amesisitza Mbatia wakati akitii agizo la kuzuia kwa mkutano wake akiwa katika Jimbo la Busokelo.

Polisi wilayani Ruangwa, Lindi hawajaeleza sababu za kuzuia mkutano huo, zaidi wamemtaka Mbatia kufika katika Kituo cha Polisi cha Lwangwa.

error: Content is protected !!