Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wamuaga rasmi IGP Mstaafu, Balozi Simon Sirro
Habari Mchanganyiko

Polisi wamuaga rasmi IGP Mstaafu, Balozi Simon Sirro

Spread the love

JESHI la Polisi Tanzania, limemuaga rasmi IGP Mstaafu, Balozi Simon Sirro leo tarehe 10 Mei  2023 baada ya kustaafu Utumishi ndani ya Jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria Machi 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Sherehe za kumuaga Sirro zimefanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dares Salaam – DPA, kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam kwa gwaride maalum kama utaratibu wa Jeshi unavyoelekeza wa gwaride maalum la Viongozi wa Polisi waliofikia cheo cha Kamishna wa Polisi na Inspekta Jenerali wa Polisi.


IGP Mstaafu, Balozi Simon Nyakoro Sirro amelitumika Jeshi la Polisi kwa miaka 30 tangu Februari 19, 1993 alipojiunga rasmi hadi kustaafu mwezi Machi, 2023 akiwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa 10 tangu uhuru wa 1961 akiongoza kuanzia Mei 28, 2017 hadi tarehe 20 Julai 2022.

Wengine waliowahi kushika nyadhifa hiyo ni ya ukuu wa Jeshi la Polisi ni IGP Mstaafu wa kwanza nchini, Elangwa Shaidi (1964 -1970), Hamza Azizi (1970 – 1973), Samweli Pundugu (1973- 1975), Philemon Maya (1975-1980), Solomon Liani (1980 – 1984), Harun Mahundi (1984-1996) Omari Mahita (1996 – 2006), Saidi Mwema (2006-2013) na IGP Mstaafu Ernest Mangu (2013-2017).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!