October 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi ‘wamtii’ Lowassa

Maelfu ya wanachama wa UKAWA waliojitokeza kumsindikiza Mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa

Spread the love

JESHI La Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam leo limelazimika kuhakikisha mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa anapata ulinzi wa kutosha. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Lowassa ameambatana na mgombea mwenza wake Juma Duni Haji kwenda kuchukua fomu katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi iliyopo katikati ya Jiji la dar es Salaam (Posta).

Mgombe huyo aliambatana na viongozi mbalimbali wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) huku akisindikizwa na maelfu ya wananchama na wapenzi wa UKAWA.

UKAWA ni Umoja wa Katiba ya Wananchi unaowakilisha vyama vinne ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD. Lowassa pia anawakilisha vyama hivyo katika safari yake ya Ikulu.

Awali kulikwepo na taarifa za kutaka kuzima maandamano hayo na kulazimisha msafara huo kwenda kuanzisha kwenye ofisi za Chadema kwa kuwa, Lowassa ni mgombea wa Chadema.

Hata hivyo, wananchi pamoja na viongozi wa UKAWA waligomea taarifa hiyo na kuongeza kuwa, wanayo haki ya kuanzia popote hivyo maandamano hayo kuanzia kwenye Ofisi za CUF zilizopo Buguruni, Dar es Salaam.

Hatua hiyo iliwalazimu polisi kuwa wapole na kutoa ushirikiano mkubwa tofauti na ilivyozoeleka. Hata hivyo, mmoja wa polisi hao alisema ‘Lowassa ni mtu mkubwa nchi hii.”

Asubuhi ya leo katika Ofisi za CUF zilizungukwa na magari ya polisi yakiwa yamebeba askari wengi huku wengine wakiwa wamebeba bunduki.

Miongoni mwa magari hayo ni pamoja na Land Rover PT 2081 likiwa na askari wa kutuliza ghasia (FFU) na Land lover PT 3386.

Akiwasili Buguruni

Kabla ya Lowassa kufika CUF, familia ya Lowassa ilitangulia na kuwasili hapo saa 5: 25. Mke wa lowassa- Regina Lowassa alikuwa katika gari aina ya VX Nisan lenye namba ya za usajili T841 CYP, na baadaye Lowassa aliingia akiwa kwenye gari aina ya Exas T878 CFU.

Wakati akienda NEC akiwa kwenye msafara, Jeshi la Polisi waliendelea na ulinzi huo hadi msafara wake ulipowasili NEC saa 7: 26 ambapo Lowassa aliingia na kuchukua fomu huku hali ikiwa shwari maeneo hayo.

Akiwa NEC, wananchi waliendelea kuongezeka wakitokea katika ofisi mbalimbali. Msafara huo pia ulionekana kuwa na mvuto kwa kila mwananchi.

Msafara wa kuondoka NEC kuelekea makao makuu ya CHADEMA ulianza mida ya saa 8:05 huku maelfu ya wananchi wakitembea wakiimba.

Katika hatua hizo zote askari waliendelea kuwa sambamba na wanachi hao pasipo vurugu hadi katika viwanja vya Biafra, Kinondoni ambapo maelfu ya watu hao walikutana kumpokea Lowassa.

Baada ya Lowassa kuongea na wafuasi aliokutana nao Biafra huku wakiwa na mabango ya kumsifu na kuikejeli CCM, alikwenda Makao Makuu ya CHADEMA ambapo safari yake iliishia hapo.

error: Content is protected !!