October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wampekua Zitto Kabwe nyumbani kwake

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini

Spread the love

IKIWA imepita siku moja tangu Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo , Zitto Kabwe kukamatwa na polisi jijini Dar es Salaam, leo Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni, limefanya upekuzi nyumbani kwake. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama cha ACT-Wazalendo na kuthibitishwa na Wakili wa Zitto, Jebra Kambole, inaeleza kuwa Mbunge huyo wa Kigoma Mjini aliwaongoza polisi hadi nyumbani kwake maeneo ya Masaki.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, baada ya polisi kukamilisha upekuzi, walimrudisha Zitto katika kituo cha Oysterbay na kwamba wakili wake anashughulikia suala la dhamana yake.

Kukamatwa kwa Zitto kumekuja siku kadhaa baada ya Jeshi la Polisi mkoani Kigoma kumtaka mwanasiasa huyo kujisalimisha polisi ili kuhojiwa kuhusu taarifa yake aliyoitoa Jumapili iliyopita, kuhusu mauaji ya askari na wananchi wa Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza.

error: Content is protected !!