Spread the love
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemchukua Halima Mdee, Mbunge wa Kawe (Chadema) kutoka polisi alikolala tangu jana na kwenda naye nyumbani kwake Makongo kufanya upekuzi, anaandika Faki Sosi.
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, Polisi hao wameenda kufanya upekuzi zaidi nyumbani kwake baada ya kuwepo kwa madai mbalimbali yanayomuhusu.
Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni siku moja baada ya Mdee kukamatwa na polisi nyumbani kwake na kuswekwa rumande kwa madai ya kuhusika kwenye vurugu za Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ulioitishwa na kughairishwa Jumamosi wiki iliyopita.
More Stories
Uchaguzi wa wanawake Chadema waingiliwa
Dk. Mwinyi amteua Dk. Mkuya, Nassor Mazrui
Waziri Majaliwa aitaka TPA kuongeza umakini