
Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, polisi wenye silaha wamezingira hospitali ya Agha Khan aliyokuwa ameenda kupata huduma ya matibabu,
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea na kumsubiri atibiwe kisha kuondoka naye.
Taarifa zinasema polisi hao wameelekea kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam ingawa haijajulikana wanapompeleka na kwa kosa gani.
Wiki iliyopita Spika Job Ndugai aliviagiza vyombo vya dola kuwakamata Kubenea pamoja na Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe na kuwafikisha mbele ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama.
TUTAWAJUZA ZAIDI
More Stories
Chadema: Serikali itoe taarifa sahihi za corona, chanjo
Othman Masoud apitia njia ya Maalim Seif
Uchaguzi wa wanawake Chadema waingiliwa