Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Polisi ‘wambeba’ mwandishi waliyemkamata kwenda Iringa
Habari Mchanganyiko

Polisi ‘wambeba’ mwandishi waliyemkamata kwenda Iringa

Spread the love

MWANDISHI wa Habari za Uchunguzi nchini Tanzania, Joseph Gandye alfajiri la leo tarehe 23 Agosti 2019, amesafirishwa kwenda mkoani Iringa. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Taarifa za awali zilieleza, Jeshi la Polisi mkoani Iringa, ndilo lililokuwa likimtaka Gandye kwa madai ya kuandika na kuchapisha habari za uongo mitandaoni kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Mwandishi wa habari hii, leo saa 12:20, alifika katika Kituo cha Urafiki, Ubungo jijini Dar es Salaam ili kujua hatua zinazochukuliwa baada ya mwandishi huyo kushikiliwa.

Alipofika kituoni hao, alimkuta polisi mwanamume ambaye hakujitambulisha jina, “nimekuja kufuata taarifa juu ya ndugu yangu aliyekamatwa jana,” mwandishi alijieleza.

“Anaitwa nani?” Polisi alihoji.

“Anaitwa Gandye, Ni ndugu yangu, aliitwa kwa mahojiano hapa jana lakini alishikiliwa mpaka sasa,” mwandishi alijibu.

“Haya subiri” polisi alimwambia mwandishi.

Baada ya mazungumzo hayo mafupi, polisi alianza kumwita Gandye, Gandye, Gandye! “ah! Hayupo hapa” polisi alimjibu mwandishi.

Baada ya mwandishi kupata majibu yaliyomwacha njiapanda, alimtafuta Jones Sendodo, Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kujua kama ana taarifa zaidi.

Wakili Sendodo ambaye alikuwepo katika mahojiano yake kituoni hapo jana, alimweleza mwandishi kwamba taarifa za leo alfajiri ni kuwa, Gandye amesafirishwa kwenda Iringa.

“Taarifa nilizonazo mpaka alfajir ya leo ni kuwa Gandye aliishasafirishwa kwenda Iringa, wameondoka alfajiri ya leo,” amesema Wakili Sendodo.

Pia mwandishi alimtafuta Chance Luoga ambaye ni Wakili wa THRDC aliyepo mkoani Iringa kujua kama ana taarifa hizo, alieleza kuwa na taarifa hizo na kwamba anafuatilia kama Gandye ameshawasili mkoani humo.

“Najua kwamba wamemsafirisha leo kabla hakujakucha, naelekea katika Kituo cha Kati cha Polisi hapa Iringa ili kujua kama wameishamfikisha ama atafika muda gani,” amesema Wakili Luoga aliyepo Iringa na kuongeza;

“Nimempigia afande hajapokea simu. Naelekea Kituo cha Kati Iringa kama hapo hatakuwepo naamini atakuwa mkoani.”

Jana tarehe 22 Agosti 2019, Gandye ambaye ni Mhariri wa Uzalishaji Maudhui na msimamizi msaidizi wa  Watetezi TV, alipigiwa simu na askari aliyejitambulisha kwa jina la Godfrey Mkude na kumtaka aripoti kwa ajili ya mahojiano katika Kituo cha Polisi Urafiki, jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuhojiwa, alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba amri ya kumkamata imetoka Iringa, hivyo kituo hicho jukumu lake ni kumhifadhi na baadaye kumpeleka Iringa kwa ajili ya taratibu zingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!