August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi walikoroga Ruvuma, wazuia vikao vya ndani vya Chadema

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limekizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya mikutano ya ndani, anaandika Irene David.

Katazo hilo limekuja siku chache baada ya viongozi waandamizi wa chama waliokuwa mkoani humo akiwamo Katibu Mkuu, Vicent Mashinji kushikiliwa na vyombo vya usalama kwa madai kwamba wanatumia lugha za kashfa na matusi kwa viongozi wa umma.

Kwa mujibu wa barua ya Kamanda wa Polisi iliyotumwa kwa Mkuu wa Mkoa huo, IGP  na Ofisa Usalama wa Taifa, ni marufuku viongozi hao kufanya mikutano ya ndani.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Gemini Mushy, amesema viongozi hao wa Chadema wanafanya shughuli zao kinyume cha sheria ya polisi sura 322 fungu 43(4).

Alisema sheria hiyo unawapa polisi mamlaka ya  kuchukua  hatua za  kuzuia shughuli kama hizo.

Kamanda huyo katika taarifa amesema viongozi hao wataruhusiwa pale  jeshi la polisi litakapojiridhisha kwamba wanafuata maelekezo yanayoendana na vikao vya ndani.

error: Content is protected !!