September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi Chadema watuhumiwa kumpiga risasi diwani wa CCM

Spread the love

VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Songwe, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Vwawa, kwa tuhuma za kumjeruhi kwa risasi, Julius Mwavilenga, Diwani wa Kata ya Sogea (CCM). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE kwa njia ya simu, George Kyando, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Songwe, amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo, usiku wa kuamkia leo tarehe 23 Novemba 2019.

“Sisi hatukamati kiongozi wa chama, tunakamata mtuhumiwa, diwani wa Sogea amejeruhiwa na risasi usiku wa kuamkia leo, na amewatambua waliomjeruhi ambao ni watuhumiwa tuliowakamata,” amesema Kamanda Kyando.

Viongozi waliokamatwa ni, Isakwisa Lupembe, Mwenyekiti wa Chadema mkoani Songwe, Joel Kilungwe, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Songwe, na Boniface Mwakabange, Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Tunduma.

Kamanda Kyando ameeleza kuwa, Mwavilenga alishambuliwa na risasi maeneo ya begani  na kwenye jicho la kushoto, na kwamba kwa sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Taarifa za viongozi hao wa Chadema kukamatwa,  zilizotolewa na asubuhi ya leo na Mdude Nyagali, Afisa Mafunzo wa Chadema Kanda ya Nyasa.

error: Content is protected !!