March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wakamata sampuli ya madini

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mwanza linashikilia lori aina ya fuso lililokuwa linasafirisha sampuli za madini 883, zilizowekwa kwenye ndoo 226 kutoka mkoani Geita kuelekea katika maabara ya kupima iliyoko jijini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Shehena hiyo ya sampuli za miamba ya madini 883 kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) ilikamatwa jana na askari wa doria.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo, amesema askari hao walikamata fuso hilo baada ya kubaini wahusika walikuwa na upungufu wa vibali vya kusafirisha mzigo kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine.

Aidha, Mongella ameagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi ili kujua uhalali wa sampuli hizo.

error: Content is protected !!