August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wajiapiza kusaka wauaji

Spread the love

JESHI la Polisi nchini limeapa kusaka na kuwatia nguvuni watu waliohusika katika mauaji jijini Dar es Salaam, Mwanza na Tanga, anaandika Happiness Lidwino.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Jiji Dar es Salaam, Advera Bulinda, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) pia Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya Polisi amesema, tayari wamekamata baadhi ya watuhumiwa wa mauaji hayo katika mikoa hiyo.

Advera amesema, kwa kushirikiana na wananchi Jeshi la Polisi limekamata watuhumiwa 14 katika matukio tofauti ndani ya Mkoa wa Mwanza. Matukio hayo ni ya watu saba wa familia moja kuuawa pia watatu waliouawa wakiwa msikitini na kwamba, uchunguzi unaendelea katika mikoa mingine.

“Tunaomba wananchi wa mikoa mingine waendelee kutoa ushirikiano kama walivyofanya wananchi wa Mwanza ambao walishirikiana na polisi kukamata wauaji 14.

“Naamini wahalifu tunawajua na tunaishi nao majumbani hivyo ni vema tushirikiane kutokomeza mauaji haya ya mara kwa mara,” amesema Advera.

Aidha, amewataka wananchi kuondoa wasiwasi kutokana na mauaji hayo na kwwamba, jeshi hilo limeimarisha ulinzi mikoa yote.

Katika hatua nyingine Advera amesisitiza wananchi kujitolea kwenda kusalimisha silaha zao na kuzisajili upya kabla zoenzi hilo halijafungwa Juni 30 mwaka huu.

“Lengo la kuhakiki kumbukumbu za silaha ni kupata taarifa sahihi juu ya umiliki wake kwa kuwa kunabaadhi ya wamiliki walishafariki na hivyo silaha zao kutumiwa vibaya na ndugu ama marafiki. Hata hivyo ni kwa mujibu wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha na risasi ya mwaka 2015 kifungu cha 66”.

Amesema, kwa kuwa ni ni juda merfu umetolewa wa kutekeleza zoezi hilo ambapo lilitangazwa tarehe Machi 21 mwa huu, atakaye kaidi atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufunguliwa mashitaka. Zoezi hilo lipo kwa nchi nzima hivyo wananchi wamesisitizwa kukamilisha.

error: Content is protected !!