Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi ‘waitikia’ msimamo wa Lissu
Habari za SiasaTangulizi

Polisi ‘waitikia’ msimamo wa Lissu

Spread the love

HATUA ya Jeshi la Polisi kufuta wito uliomtaka Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kujipeleka katika Kituo cha Polisi Moshi, Kilimanjaro unakwenda sambamba na msimamo wa mgombea huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Jana Alhamisi tarehe 1 Oktoba 2020, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lilimuandikia barua ya wito Lissu likimtaka afike katika ofisi zake leo Ijumaa saa 3:00 asubuhi kujibu tuhuma zake. 

Baada ya barua hiyo, Lissu ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa chama hicho, kikuu cha upinzani nchini, aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter akieleza, hatotekeleza wito huo na zaidi anaendelea na ratiba zake za mikutano ya kampeni.

          Soma zaidi:-

Kwenye ukurasa wake wa twitter Lissu aliandika “Wito wa polisi sio barua ya kirafiki, ni amri ya kisheria. Wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa.

“Barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama. Huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria. Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho (leo).”

Leo tarehe 2 Oktoba 2020, SACP Lazaro Mambosasa,  Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, amesema jeshi hilo limesitisha wito wake kwa Lissu likidai, limeona busara Lissu aendelee na ratiba yake.

“Jeshi la Polisi limesitisha wito huo na kumtaka Tundu Lissu kuendelea na kampeni zake za Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.”

“Jeshi la polisi limeona ni vema kutumia busara kumuacha Lissu kuendelea na ratiba zake kipindi hiki cha kampeni na kwa kuwa tayari IGP Sirro alishatoa maelekezi kwa Lissu kuripoti Kituo cha Polisi Moshi Mkoa wa Kilimanjaro. Hivyo Jeshi la Polisi Kanda Maalum limesitisha wito huo,” amesema Kamanda Mambosasa.

Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilimuandikia barua Lissu muda mchache baada ya Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro kumtaka Lissu, kuripoti Kituo cha Polisi Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

IGP Sirro alisema, Lissu amekuwa na tabia ya kukaripia na kuwagombeaza viongozi na askari polisi katika mikutano yake ya kampeni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!