January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi waendelea kumchunguza mfuasi wa Chadema

Spread the love

JESHI la Polisi Jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Idara ya ya Uhamiaji inaendelea kumchunguza mtu aliyekamatwa na hati za uraia wa nchi mbili, anayedaiwa kuwa mwanaharakati wa siasa katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Bashiri Fenele Awale Ally, amekamatwa kutokana na utata wa uraia wake na jinsi ambavyo alivyokuwa akijihusisha na masuala ya siasa nchi Tanzania.

Kamanda Kova amesama kuwa mtuhumiwa huyo mwenye hati ya kuzaliwa ya Tanzania yenye namba D063711 kwa jina la Bashiri Abdi Ally ambapo ilionyesha kuwa amezaliwa Julai 11, 1969 katika hospitali ya Dodoma.

Lakini pia mtuhumiwa huyo amekamatwa na pasi ya kusafiria ya Kenya yenye namba C000529 ambapo ilionyesha kuwa alizaliwa Nairobi Kenya Julai 11, 1969 kwa jina la Bashir Fenal Abdi Ally Awadhi.

“Kwa uchunguzi wa awali pamoja na kumbukumbu zenye utata mtuhumiwa mtajwa sio raia wa Tanzania bali ni raia wa Kenya ambaye alipeleka maombi idara ya uhamiaji lakini bado hajakubaliwa,” amesema Kamanda Kova.

Wakati huohuo, Kamanda Kova amesema jeshi hilo limekamata waharifu saba wakiwa bunduki aina ya SMG moja, bastola sita na bunduki aina ya Mark 4 Riffle moja na risasi 62.

Kamanda Kova amesema waharifu hao ambao wana viashiria vya ugaidi walipanga kuvamia vituo vya polisi lakini kabla hawajatekeleza mipango yao wamekamatwa.

Kova amesema kuwa mpaka sasa jumla ya majambazi wanahusishwa na ugaidi wamefikia 74, wamekamatwa ikiwa pamoja na silaha 51 na risasi 890 za silaha mbalimbali.

error: Content is protected !!