May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wadaiwa kuzuia kikao cha kamati kuu NCCR-Mageuzi

Spread the love

 

JESHI la Polisi Ilala, Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania, limezuia kikao cha kamati kuu ya chama cha siasa cha upinzani cha NCCR-Mageuzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kikao hicho kilikuwa kimepangwa kufanyika leo Jumamosi, tarehe 28 Agosti 2021, katika ukumbi wa Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kikao hicho kuanza kwa wajumbe kufika, polisi wenye silaha mbalimbali, wameonekana katika ukumbi huo wakizuia usifanyike.

Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-Mageuzi, Edward Simbeye amesema, maandalizi yote ya kikao chetu yalikuwa yamekamilika toka jana usiku na leo ilikuwa ni kufanya kikao tu.

“Lakini cha kushangaza, Jeshi la Polisi limekuja ukumbini saa 12:00 asubuhi na hoja yao haturuhusiwi kufanya kikao hicho na tulipowauliza walisema, shughuli zote za kisiasa zimezuiwa.”

“Sisi tuliwaeleza kwamba, kikao cha kamati kuu kipo kwa mujibu wa katiba, lakini kikao chetu ni kifupi sana na kina wajumbe 19 lakini waliokuwa wamethibitisha kuhudhuria ni 15 hivyo, ni idadi ambayo tunaweza kukaa kwa tahadhari ya corona,” amesema Simbeye.

Amesema, licha ya kuwaeleza hivyo “wao walikataa na wakawaeleza wenye ukumbi kwamba haturuhusiwi kufanya kikao. Wanatuambia wamepata taarifa kuna kikao cha watu zaidi ya 100, lakini tuwaeleze mgeni rasmi ni nani, sisi tukawaambia wasome katiba yetu, kikao cha kamati kuu kina wajumbe wasiozidi 19 lakini hawakuelewa.”

Simbeye amesema, baadaye watazungumza na waandishi wa habari ili kutoa taarifa zaidi ya nini wanakusudia kukifanya.

Jitihada za MwanaHALISI Online kuwapata jeshi la polisi ili kujua kwa nini wamezuia kikao hicho, zinaendelea

error: Content is protected !!