March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi ‘vibaka’ wapewa neno

Bahame Nyanduga, Mwenyekiti wa Haki za Binadamu na Utawala Bora

Spread the love

TUME y a Haki za Binadamu na Utawala Bora Nchini, imelionya Jeshi la Polisi na kulitaka kuagiza askari wa jeshi hilo kurudisha mali walizochukua katika kiwanda cha juisi cha Sophy kilichopo Mkuranga mkani Pwani, anaandika Angel Willium.

Kadhalika, Tume hiyo imetaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuchunguza madai ya askari Salehe Mohammed mwenye namba 8 G 5941 PC anayedaiwa kuomba rushwa ya Sh. 200,000 kutoka kwa wamiliki wa kiwanda hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nyanduga amesema, jeshi hilo liagize askari wake kurudisha au kuwalipa fidia wafanyabiasha hao kuhusu mali zoa ikiwemo mifuko ya 48 ya chupa tupu za plastic, sukari kg 50, debe za lita 30 dawa ya chungwa, pipa za platiki 4 na jenereta 1 aina ya boss.

Pia amesema mlalamikiwa Jafari Ibrahimu na Mayema Mapalala Takukulu ichunguze tuhuma zao za kuomba rushwa ya sh.3,000,000 kutoka kwa Jimmy Sanday ambaye ni mmiliki wa kiwanda hicho.

Tume imebaini kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa na askari hao kwa kuwanyanyasa na kuwadhalilisha wafanyabiashara wa kiwanda cha juice kinyume cha ibara ya 12(2), 13(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Aidha, Nyanduga amesema jeshi hilo linatakiwa liandae program itakayokuwa inawapatia mafunzo ili kuwakumbusha masuala ya haki za binadamu mara kwa mara .

Juni 4 mwaka huu wafanyabiashara wa kiwanda cha juisi cha Sophy walifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na askari wapatao 10 huku wakipora mali ikiwamo fedha kiasa cha Sh. milioni 16.5.

error: Content is protected !!