August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi tuhumani kwa mauaji Mwanza

ACP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza

Spread the love
ASKARI Polisi jijini Mwanza wanatuhumiwa kwa kumpiga na kumuua Danny Jalali, mkazi wa Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela, anaandika Moses Mseti.
Tukio hilo lilitokea tarehe 13 Juni mwaka. Kuuawa kwa Jalali kunadaiwa kutokana na kumzulumu Shilingi milioni moja mtu mmoja ambaye hajafahamika jina.
Akizungumza na Mwanahalisi Online mjane wa marehemu huyo, Rucia Chifunda amesema kuwa, alishangazwa kuona polisi wakimpiga mume wake (Danny) badala ya kufuata sheria kwa kumpeleka mtuhumiwa sehemu hisika.
Amesema kuwa, kifo mume wake kimesababishwa na polisi ambao wanapaswa kuchukuliwa hatua na wakuu wao wa polisi ili kuwa fundisho kwa askari wengine.
“Polisi walipomkamata mume wangu (Danny) na kumpiga na walipoona wamemsababishia majeraha makubwa, walimpelekea hospitalini (Sekou Toure) na baadaye walimpelekea Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) ambako alipoteza maisha,” amesema Rucia.
Baada ya polisi waliofanya kitendo hicho pia wanatuhumiwa kupokea kiasi cha Sh. 500,000 kutoka kwa Rucia wakidai ni kwa ajili ya matibabu ya marehemu.
Mmoja wa rafiki wa karibu na marehemu Danny, Kennedy Simtowe amesema, siku ambayo marehemu huyo alikamatwa na polisi, walikuwa pamoja na kwamba, baada ya kumkamata walianza kumuangushia kipigo.
Amesema kuwa, polisi hao waliokuwa wakiongozwa na WP, Salma wa Kituo cha Polisi cha Kirumba Wilaya ya Ilemela, walianza kumpiga.
“Afande Salma nilipokuwa namuomba ili nionane na ndugu yangu (marehemu Danny) alikuwa hataki na wakati mwingine wanatoa lugha chafu kwetu,” amesema Simtowe.
Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ameeleza kutambua tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi zaidi.
“Tunaendelea na uchunguzi kama ni kweli, hatua ziweze kuchukuliwa kwa polisi waliofanya kitendo hicho, kuna mambo mengine watu wanaongea sana, ngoja tuchunguze tuone,” amesema Msangi.
error: Content is protected !!