Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi Tanzania yazungumzia tukio la Mbowe
Habari MchanganyikoTangulizi

Polisi Tanzania yazungumzia tukio la Mbowe

Spread the love

JESHI la Polisi Tanzania, limetoa taarifa za uchunguzi wa awali wa tukio linalodaiwa kushambuliwa kwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Mbowe anadaiwa kushambuliwa na watu watatu usiku wa kuamkia Jumanne tarehe 9 Juni 2020 akiwa anapanda ngazi nyumbani kwake Area D jijini Dodoma.

Baada ya tukio hilo, Mbowe alipelekwa Hospitali ya Dodoma Christian Medical Center (DCMC), Ntuka.

Jioni ya siku hiyohiyo, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam anapoendelea na matibabu hadi sasa.

Leo Ijumaa tarehe 12 Juni 2020, David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania ametoa taarifa za uchunguzi wa awali wa tukio hilo akisema, baada ya taaruifa ya awali, iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Mroto, kumekuwa na simu nyingi zinapigwa na waandishi.

Amesema, waandushi wa habari wanataka kufahamu matokeo ya uchunguzi kuhusiana na taarifa iliyofikishwa katika Kituo cha Polisi Kati Dodoma.

“Napenda kujulisha Jeshi la Polisi limeendelea kufanya upelelezi wa kina kuanzia kwa mhanga mwenyewe wa tukio ambaye alidai muda wa saa saba hivi usiku akiwa kwenye ngazi ya kuingia nyumbani kwake, akiwa anatokea kwa mzazi mwenzake aitwaye Joyce Mukya Mbunge wa Viti Maalum Chadema anayeishi eneo la Medeli jijini Dodoma, alishambuliwa na kuumia kwenye mguu wa kulia,” amesema Misime.

“Mhanga wa tukio alidai, wakati anashambuliwa alipiga kelele nyingi kuomba msaada ambao aliupata toka kwa dereva wake ambaye naye alipiga simu kwa Joyce Nkya kumjulisha tukio.”

“Na hatimaye wakaamua kuomba dereva na mhanga wa tukio waondoke kwenda kwa Joyce Mukya kisha hospitali iliyoko takribani kilomita 5 nje ya Jiji la Dodoma pasipo kuona umuhimu wa kutoa taarifa Polisi kabla ya kwenda kwa Joyce Mukya na hospitali,” amesema.

Taarifa hiyo ya Polisi inasema, “upelelezi wetu umepata ushahidi wa kutosha kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu ambao kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada, na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa.”

Amesema, hata hivyo, kwa mujibu wa mashahidi hawa, hakuna hata mmoja aliyeweza kusikia kelele hizo au kuona Mbowe akishambuliwa.

“Kwa mantiki hiyo, ushahidi pekee unaozungumzia kushambuliwa ni maelezo ya mhanga wa tukio (Mbowe) pamoja na dereva wake ambayo kwa hali ilivyo sasa yanatia shaka kuhusu ukweli wa tukio hili,” amesema

Misime amesema, “mashaka hayo yanaongezeka zaidi pale tulipobaini nyumbani kwa Mbowe, alikuwemo kijana wake aitwaye James Mbowe ambaye hawakuona umuhimu wa kumjulisha kuhusu tukio lilitokea hapo nyumbani badala yake waliona umuhimu wa kumjulisha Joyce Mukya aliyekuwa mbali na eneo la tukio.”

“Uchunguzi wetu umethibitisha siku ya tarehe 8 Juni 2020, Mbowe alitembelea sehemu kadha za starehe zinazouza vileo ikiwepo Royal Village na kupata kinywaji,” amesema.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto

Misime amesema,  “hata alipofika hospitalini alionekana akiwa katika hali ya ulevi chakari kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa.”

Akihitimisha taarifa yake, Misime amesema, “tunaendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa tukio hili, hivyo tunaomba wananchi wote wenye taarifa zitakazoweza kusaidia upelelezi huu wazilete kwetu. Tutaendelea kutoa taarifa kwenu kadri ushahidi utakavyopatikana.”

Katika taarifa ya Kamanda Muroto aliyoitoa mbele ya wanahabari tarehe 9 Juni 2020 alisema tukio hilo lilitokea kati ya saa sita na robo usiku na taarifa wamezitapa saa moja asubuhi.

Muroto alisema, taarifa walizopata ni Mbowe alishambuliwa na watu watatu waliokuwa wamevalia majaketi ambapo baada ya dereva wake kumshusha, “wakati anapandisha ngazi, alikutana na watu watatu wamevaa jaketi na kumshambuliwa kwa kumkanyaga kanyanga na mateke.”

Alisema, baada ya shambulio hilo, Mbowe alipelekwa hospitalini kwa matibabu.

“Polisi tunafanya uchunguzi wa kina bila kuacha chochote. Kupata ukweli wa tukio hili. Hakuna kitu kitakachoachwa,” alisema Muroto.

“Tukio hili ni kama tukio jingine, linachunguzwa na vyombo. Tukio hili lisitumike vibaya au kisiasa au njia yoyote ya kujiongezea umaarufu kwa mtu au kundi,” alisema Kamanda huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!