April 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Tanzania yazuia mikusanyiko isiyo halali

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime

Spread the love

JESHI la Polisi Tanzania limetoa onyo la mikusanyiko ya aina yoyote katika kipindi hiki cha maombolezo ya kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Onyo hilo limetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020.

Miseme amatoa onyo hilo ikiwa ni saa chache zimepita tangu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwakaribisha Watanzania kumpokea Tundu Lissu, Makamu mwenyekiti wa chama hicho.

Lissu anatarajiwa kurejea Tanzania Jumatatu mchana tarehe 27 Julai 2020 akitokea nchini Ubelgiji ambako amekuwa huko tangu tarehe 6 Januari 2018.

          Soma zaidi:-

Katika taarifa ya Misime imesema, katika kipindi hicho, Taifa liko katika maombolezo ya hayati Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia jana Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 katika moja ya Hospitali jijini Dar es Salaam.

Soma taarifa yote ya Kamanda Misime

error: Content is protected !!