Saturday , 22 June 2024
Home Kitengo Michezo Polisi Tanzania yatoa sababu kuendelea kumshikilia Idris
Michezo

Polisi Tanzania yatoa sababu kuendelea kumshikilia Idris

Idriss Sultan
Spread the love

JESHI la Polisi nchini Tanzania, limeeleza sababu za kuendelea kumshikilia Idris Sultani, Msanii wa Vichekesho Tanzania, anayesota rumande kwa muda wa siku tano, ni uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kutokamilika. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Idris anashikiliwa katika Kituo  cha Polisi cha Oysterbay, wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, tangu tarehe 19 Mei 2020, alipojisalimisha kituoni hapo, kwa ajili ya kuhojiwa dhidi ya kosa la uonevu kwa njia ya mtandao, linalomkabili.

Msanii huyo amekumbwa na tuhuma hizo, baada ya video inayomuonesha akiicheka picha ya zamani ya Rais John Magufuli, kusambaa mitandaoni hivi karibuni.

David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, akizungumza na Mwanahalisi Online kwa  simu, leo Jumamosi tarehe 23 Mei 2020, amesema msanii huyo hajapewa dhamana kwa kuwa, uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili haujakamilika.

Misime amesema, Jeshi la Polisi haliwezi kukimbilia kumpa mtuhumiwa dhamana, wakati uchunguzi wa tuhuma zake haujakamilika.

“Kwanza niseme kwamba, ukikamatwa na polisi kwa tuhuma fulani wakati wa kukusanya ushahidi, wakati tunakuhoji tukigundua una makosa mengine tutaendelea kukuhoji nayo.  Hatuwezi kukimbilia kukupa dhamana eti kwa sababu kuna dhamana,” amesema Misime

“Lazima tukamilishe haya ambayo tunaona kwamba kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi wa kutosheleza, ili kama mtu anapoonekana kuna  ushaidi wa kupelekwa mahakamani, apelekwe mahakamani na kama hakuna ushaidi aweze kuachiwa.”

Mapema leo Jumamosi asubuhi, wakati akizungumza na Mwanahalisi Online kwa njia ya simu leo, Benedict Ishabakaki, Wakili wa Idris, amesema anaendelea kufuatilia dhamana ya msanii huyo.

“Jana walikataa kutoa dhamana, na hawajatoa sababu. Wakishakwambia hakuna dhamana ina maana kesho yake unafuatilia tena, hivyo leo nafuatilia dhamana maana wanatoa siku yoyote,” amesema Wakili Ishabakaki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ukiwa na Meridianbet ni kula pesa tu

Spread the love  Alhamisi ya leo mechi za EURO zinazidi kuendelea huku...

Michezo

Leo pesa utaipatia kwa Ureno na Uturuki ukiwa na Meridianbet

Spread the love  Kama kawaida michuano ya EURO 2024 inazidi kupamba moto...

Michezo

Leo Uingereza, Uholanzi zote kukupa pesa

Spread the love Siku ya leo EURO 2024 kupigwa katika viwanja mbalimbali,...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

error: Content is protected !!