Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi Tanzania: Tunaendelea kuchunguza tuhuma za Nabii Mwingira
Habari Mchanganyiko

Polisi Tanzania: Tunaendelea kuchunguza tuhuma za Nabii Mwingira

Kiongozi wa Kanisa la Efatha, Mtume na Nabii Josephat Mwingira
Spread the love

 

JESHI la Polisi Tanzania limesema, Kiongozi wa Kanisa la Efatha, Mtume na Nabii Josephat Mwingira alikwisha kufika na kuandika maelezo juu ya tuhuma alizozitoa dhidi ya Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa aliyoitoa leo Ijumaa, tarehe 30 Desemba 2021, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime, “Askofu Mwingira alishafika polisi na kuandika maelezo yake.”

“Hatua zinazoendelea tangu atoe maelezo hayo ni kufanyika kwa uchunguzi wa aliyoyaeleza,” ameongeza Misime.

David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi

Hata hivyo, taarifa hiyo haikufafanua Nabii Mwingira alihojiwa linin a wapi na kwa maelezo ya awali, nini wamekibaini.

Nabii Mwingira anatuhumiwa kutoa tuhuma nzito za kunusurika kuuawa mara tatu na watu wa serikali jambo lililomfanya Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene kuagiza Polisi kumtafuta na kumhoji kuhusu tuhuma hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!