
Hamza Mohamed, aliyefyatulia risasi Polisi na kuwaua
JESHI la Polisi nchini Tanzania limesema, Hamza Mohamed aliyewaua askari polisi watatu na mlinzi mmoja wa kampuni ya SGA kisha kuuawa, alikuwa ni gaidi aliyejitoa kuifia dini. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah, TUDARCo … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 2 Septemba 2021 na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.
Alikuwa akitoa taarifa ya uchunguzi wa awali wa tukio hilo lililotokea tarehe 25 Agosti 2021 katika makutano ya barabara ya Kinondoni na Kenyatta jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo, Hamza aliwaua askari hao kwa bastola yake kisha akachua silaha walizokuwa nazo polisi na kuanza kufyatua risasi hovyo karibu na Ubalozi wa Ufaransa kabla ya yeye mwenyewe kuuawa na polisi.
Askari hao waliouawa; ni Miraji Khatib Tsingay, Emmanuel Keralya, Kangae Jackson na mlinzi wa SGA Joseph Okotya Mpondo.

DCI Wambura amesema “tumebaini, Hamza Mohamesd ni mtu ambaye amekuwa akiishi kisiri lakini akiwa na viashiria vyote vya kigaidi. Hamza alikuwa ni gaidi wa kujitoa mhanga.”
“Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo ya kigaidi inayoonesha vitendo vya vikundi kama IS,” amesema
Amesema, tabia zake na matendo yake kwa kipindi kirefu ameyapata kupitia mawasiliano na baadhi ya nchi rafiki zenye matendo ya kigaidi.
“Tumechunguza kwa kina yale yote yanayomhusu Hamza Mohamed. Hakuwa na madini wala fedha wala hakuwa anamiliki migodi Chunya (mkoani Mbeya). Hamza alikuwa ni magadi walioamua kuifia dini,” amesema.
More Stories
Huduma ya Teleza Kidigitali yazinduliwa Morogoro
Taasisi yaanzisha mafunzo kuwanoa wadau wa mawasiliano nchini
Wabunge upinzani, CCM waungana kumpongeza Rais Samia