October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Tanga wazuia mkutano ACT-Wazalendo

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo akisaini kitabu katika Ofisi ya Mkuu wa Polisi mkoa wa Tanga, mara baada ya mkutano wake kuzuiwa

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Tanga limezuia Chama cha ACT-Wazalendo kufanya mkutano wake wa ndani. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taraifa ilizofikia MwanaHALISI Online na kudhibitishwa na kamati ya maandalizi ya mkutano huo zimeeleza kuwa, mkutano wa ndani uliopangwa kufanywa leo tarehe 4 Aprili 2019 umezuiwa.

Hata hivyo, Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo-Taifa amesema, ‘polisi wamezuia mkutano wetu Tanga’. Mkutano huo uliopangwa kufanyika katika Ukumbi wa Hindu Mandali jijini humo.

Mratibu wa ziara ya viongozi wa ACT-Wazalendo mkoani Tanga, Mbarara Maharagande ameauambia mtandao huu kwamba, Jeshi la Polisi limezuia mkutano huo bila kueleza sababu zozote.

“Ndio tunashughulikia nipige baadaye kidogo, baada ya dakika ishirini nipigie tena, kiongozi mkuu wa chama atatoa taarifa kamili,” amesema Maharagande ambapo taariza za jana zinaeleza kuwa, jeshi hlo lilikuwa limeruhusu.

Chama hicho kilipanga kufanya ziara ya siku mbili mkoani Tanga, kuanzia leo hadi kesho tarehe 5 Aprili 2019 ambapo ziara hiyo ilipangwa kuanza Tanga Mjini na kumalizia Wilaya ya Pangani.

Katika ziara hiyo, Zitto Kabwe pamoja na mwanachama mpya wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamad walipanga kufanya vikao vya ndani vya kukiimarisha chama hicho.

Miongoni mwa shughuli zilizotarajiwa kufanywa na chama hicho leo ni pamoja na na kuwapokea madiwani 10, wenyeviti wa serikali za mitaa 62, ambao hawajaweka bayana wanatokea vyama gani, kufungua matawi 81 na kupokea wanachama wapya 7,641.

error: Content is protected !!