Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi shirikianeni na wananchi kubaini magaidi – Rais Samia
Habari za Siasa

Polisi shirikianeni na wananchi kubaini magaidi – Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameliagiza Jeshi la Polisi, lishirikiane na raia katika kuwabaini watu wanaojihusisha na vitendo vya ugaidi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Amri Jeshi huyo mkuu wa Tanzania, ametoa agizo hilo leo Jumatano, tarehe 25 Agosti 2021, akifungua kikao kazi cha maafisa wakuu waandamizi na makamanda wa Polisi wa mikoa wa jeshi hilo, Oysterbay, mkoani Dar es Salaam.

Ameliagiza jeshi hilo lijenge urafiki wa karibu na raia, ili watoe ushirikiano wa kuwafichua watu hao wanaokaa katika makazi yao.

“Kuna suala jingine la jeshi kuwa ndani ya makazi ya raia kutokana na mawimbi ya kuenea ugaidi, haya magaidi sasa wanambinu ya kukaa ndani ya raia huko mitaani. Wanajichanganya tu, inawezekana unakaa naye nyumba moja lakini humjui huyu ndiye,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “sasa hii inatufanya jeshi tukajenge urafiki kwa raia, ili raia wawe na moyo na imani ya kutuambia nani ni nani katika maeneo yao. Tukitegemea wenyeweviti wa mitaa huenda tukakosa taarifa.”

Aidha amesema, jukumu la ulinzi na usalama katika makazi ya raia halipaswi kuwa la Polisi jamii peke yake, bali Askari Polisi wanatakiwa kujenga urafiki wa karibu na wananchi.

“Badala ya kuwafanya Polisi jamii nao washike virungu usiku wasaidie kulinda, kuwe na Polisi jamii kujua nani ni nani na hicho ndicho kinasumbua nchi jirani.”

“Wahahalifu wako ndani ya jamii na jamii wasipokuwa na imani na jeshi hawatoi taarifa, lakini wakiwa na imani watatoa taarifa na kuwachukua kirahisi,” amesema Rais Samia.

Pia, Rais Samia amewaagiza maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, kushiriki vikao vya ulinzi na usalama vinavyofanyika katika nchi jirani, ili kujua hali ya usalama wa mipaka ya nchi.

“Vikao vya ulinzi na usalama jirani na vyenyewe nahamasisha, si kwa fujo nita-control (dhibiti) hizo safari, lakini tuweke sawa tuone nchi yetu inakuwa salama, hili ni kwa vyombo vyote na si Polisi,” amesema Rais Samia.

Wakati huo huo, Rais Samia ameagiza Askari Polisi kukwepa kuishi katika makazi ya raia, ili kujiweka mbali na vitendo vya ushawishi.

“Kupanga kwao au kukaa kwao mitaani kunawafanya wazoeleke na jamii na hata kama mhalifu jirani yake au amepanga naye nyumba moja, atasita sana kumsema kwamba huyu mhalifu. Hilo nalo mliangalie,” amesema Rais Samia.

“Kwenda kwa jamii sawa lakini mnakwendaje? Sio kwenda kabisa kabisa, kule kwetu mkipeleka wanajeshi au askari wakifika tuna muangalia interest yake ni nini, siku ya tatu tunampa mchumba akioa kazi imekwishia hapo, hafanyi sababu ni mmoja wa ukoo ule.”

2 Comments

  • Huu si sawa na ujasusi? Askari anakaa uraiani akipeleleza kinachosemwa na kutendwa. Raia wakishamgundua wanampiga pande

  • Tusichanganye gaidi na jambazi. Hawa ni watu tofauti kabisa na mbinu za kuwabana pia ni tofauti

    Haya maneno ya mchumba ni gumzo la kijiweni.Tuwe serious

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!