July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Mwanza: Tumepata picha ya mtuhumiwa

ACP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mwanza limedai kupata picha ya mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi, anaandika Moses Mseti.

Mtu huyo anadaiwa kufanya uhalifu wa kutumia silaza za moto katika miamala inayofanywa kwa kupitia mitandao ya simu za mkononi kwa wakati tofauti.

Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ahmed Msangi ambaye pia ni Kamanda wa Polisi mkoani humojana amedai kuwa, mtuhumiwa huyo ndiye kinara wa matukio ya uhaifu wa kutumia silaha za moto Jijini humo.

“Hata katika tukio la hivi karibuni (Mei 5 mwaka huu) lililotokea katika Kata ya Kishiri (Igoma), watu wanne wanaosadikika majambazi waliopora Sh. 2 milioni na kujeruhi watu wawili na huyu (anaonesha picha) ni mhusika wa tukio hilo na ndiye kinara mkuu,” amedai Msangi.

Kamanda Msangi amesema kuwa, kutokana na kuwepo kwa matukio mengi katika mkoa huo ambao ni wa pili kwa uchangiaji wa pato la Taifa, ameapa kupambana ili kuvunja mtandao huo.

Katika kipindi cha miezi miwili mpaka sasa kumekuwepo na matukio saba yanayohusiana na uvamizi wa maduka ya yanayofanya miamala ya fedhwa kwa njia ya simu.

Tukio la kwanza lilitokea katika Kata ya Igogo ambako wavamizi waliua na kupora, tukio lingine lilitokea Ngaza Nyegezi ambako dereva bodaboda kuawa.

error: Content is protected !!