August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Morogoro wamnasa muuaji

Spread the love

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro, linamshikilia kijana Rashidi Hassan (20), mkazi wa wilaya ya Kilosa, kwa tuhuma za kufanya mauaji baada ya kumpiga mwenzake na kitu butu mwilini, anaandika Christina Haule.

Ulrich Matei, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, amesema tukio hilo lilitokea 29 Agosti, mwaka huu, saa 7:40 mchana katika eneo la Msamvu, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda Matei amewambia wanahabari kuwa, kijana huyo alimshambulia kwa kitu butu bwana Hassan Hans mwenye umri wa kati ya miaka 30-35 na kusababisha kifo chake baada ya kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa mkoani hapa.

Mwili wa marehemu Hassan, umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya kufanyiwa utaratibu wa maziko.

Hata hivyo, kamanda Matei amesema kuwa, upelelezi wa tuhuma hizo unaendelea kufanyika licha ya mtuhumiwa huyo kudaiwa kuugua ugonjwa wa akili kwa sasa, tatizo ambalo wanasubiri majibu kutoka kwa madaktari kuthibitisha kabla ya kumfikisha mahakamani.

 

error: Content is protected !!