August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Moro wanasa dawa za kulevya

Spread the love

POLISI mkoani Morogoro, imemkamata Bwiru Hamisi (44) mkazi wa Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kusafirisha kilo 60 za dawa za kulevya aina ya bangi kutoka Doma wilayani Mvomero kwenda jijini Dar es Salaam, anaandika Christina Haule.

Ulrich Matei, Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, amesema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe 5 Septemba, mwaka huu saa 1:00 asubuhi katika eneo la Mindu, barabara kuu ya Morogoro inayokwenda Iringa.

Kamanda Matei amesema kuwa, askari polisi walikamata bangi kilo 60, zilizokuwa zinasafirishwa kwa kuwekwa kwenye buti ya gari yenye namba za usajili T 734 CUG huku ikiwa kwenye mfuko wa sandarusi.

“Mtuhumiwa huyo alikuwa amehifadhi bangi hiyo kwenye mifuko mitatu tofauti ya sandarusi, akitokea eneo la Doma Wilayani Mvomero kuelekea jijini Dar es Salaam na kwamba inadaiwa kuwa huenda mtuhumiwa huyo akawa mtumiaji wa madawa hayo na pia ni muuzaji,” amesema.

Hata hivyo Kamanda huyo amesema, mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika.

error: Content is protected !!