August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Moro wanasa bunduki tatu mitaani

Ulrich Matei Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro

Spread the love

JESHI la Polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia watu 12 baada ya kuwakamata wakiwa na silaha tatu za aina mbalimbali ikiwemo bunduki y kivita aina ya AK 47, anaandika Christina Haule.

Ulrich Matei Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amesema watuhumiwa hao walikamatwa na bunduki moja aina ya AK 47 ikiwa na riasasi 19 pamoja na zingine mbili aina ya Shotgun zenye risasi 4,  zote zikimilikiwa kinyume cha sheria.

Matei amesema kuwa walifanya msako mkali baada ya kuata taarifa za kiintelijensia kutoka kwa raia wema ya kwamba kuna watu wanaomiliki silaha isivyo halali.

“Tarehe 24 Desemba saa moja usiku katika kata ya Mang’ula wilayani Kilombero tulikamata AK 47 yenye Na. KO 363394 ilikuwa imehifadhiwa kwenye begi nyumbani kwa mwanamke mmoja ambaye alifanikiwa kutoroka mara baada ya kuona askari wakielekea nyumbani kwake.

Siku hiyo hiyo majira ya saa 11 alfajiri katika kata ya Kidodi polisi pia walimkamata mtuhumiwa mmoja ambaye anakadiriwa kuwa na miaka 54 baada ya kumkuta na silaha aina ya Shotgun isiyokuwa na namba, na risasi 4 zilizohifadhiwa kwenye nguo na kufichwa pangoni,” amesema Kamanda Matei.

Tukio lingine lililotokea, limemuhusisha mwanaume mwenye umri wa miaka 52 aliyekamatwa Desemba 25 katika tarafa ya Vigoi wilayani Ulanga akiwa na silaha aina ya Shortgun yenye Na. 0648 bila kuwa na kibali cha umiliki. Alikuwa ameificha chini ya kitanda ndani ya chumba anachoishi.

Kamanda Matei amesema majina ya watuhumiwa hao yamehifadhiwa kutokana na sababu maalum ambapo kwani wanaendelea kuhojiwa huku jitihada za kumtafuta mwanamkea aliyekimbia zikiendelea na kwamba watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

error: Content is protected !!