December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Mbeya wamsaka dereva wa lori

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mbeya linamsaka dereva wa lori la mafuta linalomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Oil Com, baada ya lori hilo kukutwa limebeba vipodozi vilivyopigwa marufuku kuingia nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo ya Jeshi la Polisi Mbeya imekuja baada ya kukamata lori hilo maneneo ya Mbarali jijini Mbeya, likiwa limebeba katoni mbili za pome kali pamoja na katoni 15 za vipodozi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo tarehe 9 Oktoba 2018, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, ameeleza kuwa lori hilo limekamatwa jana majira ya saa nane mchana likitokea nchini Zambia.

“Lori hilo lenye namba za usajili T 233 CXL limekamatwa na polisi eneo la Mbarali jijini hapa, jana saa nane mchana, likitokea nchini Zambia,” amesema Kamanda Matei.

error: Content is protected !!