July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi, majambazi watunishiana misuli

IGP Ernest Mangu

Spread the love

HALI ya usalama leo  katika Kata mpya ya nyegezi Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, iligubikwa na hofu kubwa baada ya jeshi la Polisi na watu watatu wanaodaiwa majambazi kurushiana risasi na katika tukio hilo jambazi mmoja kufariki. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea)

Tukio hilo ambalo lilitokea  nje ya  kambi ya jeshi la wananchi (JWTZ), baada ya wananchi wa eneo la Igubinya kuwatilia shaka watu watatu ambao wanadaiwa majambazi.

Hata hivyo baada ya wananchi hao kutoa taarifa kwa jeshi la polisi waliofika katika eneo hilo la tukio na kuanza kuipambana na majambazi hao waliokuwa na silaa aina ya Smg, katika mapambano hayo jambazi mmoja aliuwawa na wawili kukimbia kusikojulikana. 

Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza na waandishi wa habari, wamesema watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi walifika katika eneo hilo kwa muda mrefu na walipojaribu kuwahoji walijibu kwajeuri. 

Hata hivyo wamesema kuwa baada ya kuona watu hao wanazunguka katika eneo hilo kwa muda mrefu walitoa taarifa Polisi na kufanikiwa kuuwa jambazi moja na wengine wawili kukimbilia kusikojulikana. 

Mashuhuda hao waliwaambia waandishi wa habari kuwa kati ya majambazi hao watatu mmoja alikuwa ni mwanamke ambaye alifanikiwa kukimbia na kusababisha hofu kwa baadhi ya wananchi wa eneo la Igubinya.

“Tulipokuwa tunajaribu kuwahoji kwa nini mnapita pita hapa kila muda na mnaonekana ni wageni wa eneo hili, majibu yao yao yalikuwa ya jeuri na kiburi ndipo tulifahamu hao watu sio watu wema na kujaribu kuwasiliana na Polisi na walipofika walipamba nao kwa silaa,” amesema Magesa mmoja wa shuhuda hao. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishina Mwandamizi Msaidizi, Charles Mkumbo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambamo walifanikiwa kukamata silaa aina ya SMG, risasi 19 ambazo hazijatumika pamoja na risasi 24 zilizotumika katika eneo la tukio.

Mkumbo amesema kuwa slaa hiyo waliokamata alikuwa nayo jambazi aliyefariki na  ambaye hajafahamika jina lake mara moja kutokana na mwili wake kupigwa risasi vibaya,ikiwemo eneo la shigo ambalo risasi lilipita na kutokezea sehemu nyingine.

error: Content is protected !!