September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi: Majambazi sugu wauawa Vikindu

Spread the love

POLISI jijini Dar es Salaam imesema watuhumiwa wanne wa ujambazi sugu waliokuwa wakishikiliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, wameuawa, anaandika Pendo Omary.

Taarifa ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliyoitoa leo imetaja idadi tu lakini sio majina wala walikokuwa wakiishi.

Kamishna Sirro amesema watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 3 Septemba 2016 kwa kutumia Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi wa kutumia silaha ambacho kimekuwa katika msako mkali wa kunasa majambazi sugu wakiwemo waliohusika na matukio ya wizi wa fedha katika benki ya Habib African na Stanbic, zote za jijini Dar es Salaam mwaka 2014.

Katika kukamatwa kwao, Kamishna Sirro amesema watuhumiwa wote walikiri kushiriki matukio ya uhalifu wa kutumia silaha na kwamba polisi imefanikiwa kukamata aina mbalimbali za silaha kufuatia ushirikiano waliotoa watuhumiwa hao.

Alizitaja silaha hizo kuwa ni bunduki 23, risasi 835, Bullet Proof tatu, sare za polisi, pingu 48 na Radio Call 12.

Akielezea namna watuhumiwa hao walivyouawa, Sirro amesema “Baada ya mahojiano zaidi majambazi hao walisesema sila hizo wamezificha huko Vikindu Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. Ndipo askari walipoambatana na watuhumiwa hao hadi kwenye msitu wa Vikindu.
“Walipofika eneo walilodai ni karibu na zilipo bunduki walishuka kwenye gari na kuingia porini watuhumiwa wakiwa wametangulia wakiwaongoza askari.

“Wakiwa msituni ghafla walisikia milio ya risasi ikitokea mbele ambapo askari walilala chini huku zikisikika sauti ‘mmetuua sisi’,” ameeleza Sirro.

Amesema baada ya risasi za mfululizo kutulia askari waliwashuhudia majambazi hao ambao walichelewa kulala chini wakati risasi zinapigwa wakiwa wamejeruhiwa sehemu za kifuani na tumboni huku wakivuja damu nyingi.

“Askari walipiga risasi kuelekeza eneo zilikotokea risasi na walipoendelea kusonga mbele walikuta silaha aina ya SMG ikiwa imetelekezwa na haikuwa na risasi ndani ya magazine hivyo kufanya idadi ya silaha za smg kufikia nne.

“Lakini majambazi wote walifariki wakiwa njiani kutokana na kutokwa na damu nyingi,” ameeleza Sirro.

error: Content is protected !!