Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Polisi laua watatu, lakamata silaha
Habari Mchanganyiko

Polisi laua watatu, lakamata silaha

Spread the love

JESHI la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es salaam limeua watu watatu wanaodai kuwa majambazi na kukamata silaha mbili aina ya Shortgun na Bastola. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi mkoani humo leo tarehe 29 Agosti 2019, amewaambia waandishi wa habari kuwa mnamo tarehe 25 Agosti 2019 walikamata silaha hizo mbili.

Na kwamba walimkamata mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la Omary Athumani (35) Maarufu ‘Danga,’ mkazi wa Mkuranga ambaye pia alikuwa anatafutwa kwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Amesema, katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, alikiri kujihusisha na matukio hayo na kuwa amewahi kufungwa miaka 30 ambapo alitolewa baada ya kukata rufaa na kushinda kisha kujiunga na kundi lingine la ujambazi.

“Mtuhumiwa huyo pia alieleza kuwa, kuna wenzake watatu ambao anashirikiana nao pia wamepanga wakavamie na kupora duka la M-pesa lililopo maeneo ya Pugu shuleni hivyo yuko tayari kuwapeleka Askari eneo la tukio.

“Kikosi kazi wakiwa na mtuhumiwa, waliweka mtego na ilipofika muda huo eneo la Pugu, washirika wake walijitokeza kutoka kwenye kichaka wanakoficha silaha na walipogundua kuwa wanafuatiliwa na askari  maeneo hayo, ghafla walianza kurusha risasi kuelekea kwa askari na mtuhumiwa alianza kupiga kelele na kujaribu kuwakimbia askari,”amesema.

Kamanda Mambosasa amesema, askari walijibu mapigo na walifanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu ambao ni Omari Athumani na wengine wawili waliofahamika kwa majina yao maarufu ‘Fullsaba’ na ‘Babu Shobo’ na mmoja aitwaye ‘Dogo Side’.

“Majeruhi wote walikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu lakini baada ya daktari kuwapima, alithibitisha kuwa wameshafariki dunia,” amesema Kamanda Mambosasa.

Amesema, baada ya upekuzi majambazi hao walipatikana na silaha mbili No. YA- 1547 aina ya Shortgun, iliyokatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi tatu, ganda moja la risasi na Bastola moja iliyofutwa namba ikiwa na risasi mbili na maganda mawili (2) ya risasi.

“Silaha aina ya Shortgun ilibainika kuwa iliporwa tarehe 13 Aprili 2019 saa nne na nusu usiku, kesi ya unyang’anyi ilifunguliwa kituo cha Ukonga na silaha hiyo ilikuwa mali ya kampuni ya ulinzi iitwayo Alems Security Co.Ltd.

“Kampuni hiyo ipo njiapanda ya Segerea Dar es Salam na ilitumika kupora kiasi cha pesa Milioni 6 huko Markaz, Gongo la Mboto kwa mfanyabiashara  Justine Chaula, pamoja na simu tano tofauti.” amesema.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, awali mtuhumiwa alikiri yeye na wenzake wamewahi kushtakiwa kwa makosa ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha, zaidi ya kesi sita ambazo zilikuwa mahakamani kabla ya kutoka kwa rufaa mwaka 2017.

Katika tukio lingine, Juni mwaka huu walipora maduka ya M-pesa, Tigo pesa maeneo ya Mazizini Ukonga, Mbezi Juu wilayani Ubungo na walipora Sh 800,000 kwa mfanyabiashara wa mchanga, maeneo ya Machimbo wilaya ya Mkuranga.

Na kwamba, polisi Wilaya ya Mkuranga ilifanya upekuzi nyumbani kwa marehemu Omary Athuman ‘Danga’ na kufanikiwa kukamata risasi saba za silaha aina ya Shorgun na kwamba, jalada la shauri hilo linapelelezwa.

“Kikosi kazi kinaendelea na msako mkali ili kuhakikisha jambazi aliyetoroka kwenye eneo la tukio, anakamatwa haraka na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

“Wananchi waendelee kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuliweka jiji letu la Dar es salaam katika hali ya amani na utulivu, ili raia wema waendelee kufanya kazi za kuinua kipato chao na taifa kwa ujumla,”amesema.

Mambosasa amesema, katika tukio la lingine, Polisi Dar es Salaam wamefanikiwa kumkamata Elia Kituli (55) mkazi wa Kivule, Wilaya ya Ilala akituhumiwa kufanya ujambazi.

Amesema, mtuhumiwa huyo alikuwa anatafutwa baada ya kukimbia kwenye tukio la ujambazi lililotokea tarehe 4 Julai 2019, ambapo majambazi wawili waliuwawa na kupatikana silaha mbili aina ya bastola Kitunda Machimbo, jijini Dar es Salaam.

“Jambazi huyo alikamatwa akiwa na silaha moja aina ya Rifle yenye namba MK3-90893 ikiwa na risasi 3 ndani ya kasha (magazine).

“Pia alikutwa na vifaa mbalimbali vilivyoporwa maeneo mbalimbali vikiwemo Ipad mbili aina ya Samsung na Apple, Smart phone 8 aina ya INFINIX, Samsung, Nokia, Huawei, Techno na Iphone, Saa moja ya mkononi aina ya Seiko 5 rangi ya dhahabu, Kisu kimoja, Digital camera moja aina ya Sony, Lap top moja aina ya Toshiba, Head phone moja na charger mbalimbali za simu,”amesema.

Amesema, mtuhumiwa wakati akiendelea kuhojiwa kituoni, aliugua ghafla na kupelekwa Muhimbili na baadaye alifariki dunia kwa maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yatoa msaada wa mil. 20 kwa waathirika mafuriko Hanang

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) sambamba na wafanyakazi wa...

Habari Mchanganyiko

Polisi wadaka mirungi kwenye basi la Extra Luxury

Spread the loveJeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limekamata shehena ya dawa za...

Habari Mchanganyiko

Oryx yaungana na jamii kuwafariji waathirika maporomoko Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeungana na Watanzania kutoa pole...

Habari Mchanganyiko

Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil...

error: Content is protected !!