July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kifo cha Fidel Odinga, madaktari kutoa majibu wiki sita zijazo

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyetta (katikati) akisaini kitabu cha maombelezo cha msiba wa mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, Fidel Odinga. wanaoshuhudia ni Odinga (kushoto) na mke wake, Ida Odinga

Spread the love

UPDATE 16:58

WAKENYA pamoja na familia ya Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga wanapaswa kusubiri kwa wiki sita ili kupata matokeo ya uchunguzi wa kinachoweza kusababisha kifo cha Fidel Odinga, baada ya uchunguzi wa awalikushindwa kutoa majibu.

Madaktari wachunguzi wa magonjwa wamekubaliana kwenda hatua ya pili ya uchunguzi kubaini kama kuna sumu yoyote (Toxicology) inayoweza kusababisha kifo chake, pia unachunguza viungo/seli (Histology) vya maiti hiyo kuona kama watagundua tatizo kwenye viungo/seli hivyo.

Katika uchunguzi huu sampuli 19 zimekusanywa na utafiti una lengo la kubaini kemikali au vimelea vinavyoweza kusababisha mabadiliko ndani ya mwili na hivyo kusababisha kifo.

Utafiti huu utafanyika nchini Kenya, na kuna sampuli zitakazopelekwa na familia nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Kwa sampuli zinazofanyiwa uchunguzi ndani ya Kenya, vaadhi zitafanyiwa uchunguzi na ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na nyingine zitafanyika kwenye maabara binafsi.

Daktari mkuu wa elimu ya magonjwa (Pathologist) wa serikali, Dr Dorothy Njeru alisema majibu ya vipimo hivyo yatapatikana ndani ya wiki sita.

UPDATE: 10:36

MADAKTARI wa sayansi ya elimu ya magonjwa (Pathologists) wameamua kufanya uchunguzi mwingine wa kimaabara leo Jumatano Januari 7, 2015 ili kubaini ni nini kinaweza kupelekea kifo cha Fidel Odinga.

Siku ya Jumanne madakatari hao wakiongozwa na Dorothy Njeru, daktari mkuu wa elimu ya magonjwa wa serikali, akiambatana na Profesa Emily Rogena kama daktari wa familia walishindwa kubaini chanzo cha kifo hicho baada ya kufanya upasuaji wa maiti hiyo (Autospy), upasuaji na ukaguaji uliochukua masaa kumi

“Ukaguaji wa maiti na upasuaji haukuweza kuleta jibu juu ya sababu inayoweza kupelekea kifo chake”, Dr. Njeru alisema.

Habari ya awali

Fidel Odinga, mtoto mkubwa wa mwanasiasa wa chama kikubwa cha upinzani cha Kenya, Raila Odinga amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha siku ya Jumapili. kifo hicho kilimkuta akiwa nyumbani kwake kwenye makazi ya watu wenye uwezo huko Bel Air-Karen katika jiji la Nairobi. Kifo hiki kimepelekea uchunguzi mkubwa unaofanywa na Jeshi la polisi huku kukiwa na ukamataji wa watu watakaosaidia jeshi la polisi katika upelelezi.

Kwa mujibu wa Peter Mungai, CID wa kituo cha Kilimani watu watatu wametoa maelezo kuhusiana na mienendo ya Fidel kabla ya kifo chake. Vile vile amesema watu kadhaa watahojiwa ikiwa ni pamoja na marafiki zake ili kujua nini hasa kimetokea.

Wakati huohuo kwa mujibu wa James Orengo, seneta wa Siaya, uchunguzi huu umepangwa kufanyika leo siku ya Jumatatu kati ya saa nne na saa tano asubuhi.

Fidel (41) alishaonekana na wachunguzi wa mambo ya kisiasa kuwa na nafasi kubwa ya kuwa mwanasiasa na hivyo kuwa kwenye nafasi ya kuweza kumrithi baba yake.

Kifo cha Fidel kilitokea baada ya kurudi nyumbani mapema siku ya Jumapili mnamo saa nane na nusu hivi za usiku akitokea kwenye starehe za unywaji akiwa na rafiki zake kwa kuamua kulala kwenye chumba cha kulala wageni ili kutomsumbua mkewe na mtoto mdogo waliolala kwenye chumba ‘kikubwa’ na siku ya Jumapili alikutwa na mke wake Lwam Getachew Bekele kitandani akiwa amekufa.

Kufuatia kifo hiki Rais wa Kenya Uhuru Kenyata na msaidizi wake William Ruto walituma salamu za rambirambi kwa Raila Odinga.

Odinga Waziri Mkuu aliyepita, anayeongoza muungano wa upinzani unaoitwa Coalition for Reforms and Democracy (CORD), ni mwanasiasa na mpinzani anayezungumzwa sana na ni mwiba kwa serikali iliyopo madarakani. Mwezi uliopita aliongoza changamoto ya kukataa sheria ya ugaidi kwa kile alichokiita ina utata kwa kulaumu kuwa serikali ya Kenya itakuwa ya kigaidi endapo sheria hiyo itapitishwa.

Mvutano wa upitishaji wa sheria hiyo ulitokea bungeni na hivyo kusababisha fujo kati ya wabunge wa serikali ya muungano na wapinzani.

Hata hivyo siku ya Ijumaa sehemu kuu nane za sheria hiyo iliyosainiwa na Rais zimetenguliwa na George Odunga Jaji wa Mahakama Kuu ili uchunguzi makini ufanyike juu ya sheria hii. Sababu za kusitishwa utumikaji wa sehemu hizo inatokana na uingiliaji wa haki za binaadamu na kwenda kinyume na katiba ya nchi.

Sheria hiyo inatoa nguvu na mamlaka kwa serikali kukamata watuhumiwa wa ugaidi ikiwa ni pamoja na kuwashikilia watuhumiwa kwa mwaka mzima bila ya kushitakiwa mahakamani. Sheria hiyo hiyo inatishia waandishi wa habari kwa kuwafunga mpaka miaka 3 endapo habari zao zitadhoofisha uchunguzi au upelelezi uliofanywa na serikali dhidi ya ugaidi.

Vipengele vingine kwenye sheria hiyo vilivyoondolewa ni pamoja na udhibiti wa wahamiaji (wakimbizi) kwa kuweka kiwango maalumu watakaokubaliwa kuwepo na tafsiri ya magaidi.

Hata serikali ilitetea sheria hiyo ni muhimu na ingeweza kudhibiti mashambulizi yanayofanywa na Al Qaeda wa Kisomali waliojiunga na wapiganaji wa al-Shabab.

Habari hii imetafsiriwa na Benedict Kimbache kutoka vyanzo mbalimbali.

error: Content is protected !!