June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi India washambuliana kwa risasi, saba wauawa

Waziri Mkuu wa Jimbo la Assam, Himanta Biswa Sarma, akiaga miili ya Polisi waliofariki dunia katika mapigano hayo

Spread the love

 

ASKARI Polisi saba wamefariki dunia huku 50 wakijeruhiwa nchini India, katika mashambuliano ya risasi ya wenyewe kwa wenyewe , yaliyoibuka Jumatatu, tarehe 26 Julai 2021, kwenye Mji wa Vairengte nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Tukio hilo lisilo la kawaida limetokea baada ya Polisi katika majimbo ya Assam na Mizoram, yaliyoko Kaskazini Mashariki mwa India, kurushiana risasi, hatua iliyotokana na mgogoro wa muda mrefu wa mipaka ya majimbo hayo.

Mgogoro huo ulishika kasi mwezi mmoja uliopita, baada ya Polisi wa Jimbo la Mizoram, kudai kwamba Polisi wa Jimbo la Assam, wamejiongezea eneo la mpaka.

Waziri Mkuu wa Jimbo la Assam, Himanta Biswa Sarma, ameshutumu mapigano hayo akisema Polisi wa Mizoram hawakupaswa kutumia nguvu, katika kukabiliana na mgogoro huo.

 

“Kwa moyo mzito tunalazimika kutambua kwamba kile kinachotajwa na upande wa Mizoram, kama kuingilia na uchokozi wa Assam kumesababisha wafanyakazi wa Polisi kupoteza maisha na zaidi ya 50 kujeruhiwa. Hii ni ya kusikitisha,” ameandika Sarma katika ukurasa wake wa Twitter.

Kufuatia mgogoro huo, Serikali za majimbo hayo, zimemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani wa India, Amit Shah, kuingilia kati ili suluhu ipatikane.

Mgogoro huo ulianza kuibuka baada ya Mizoram kujitenga na Assam 1986, baada ya kupewa mamlaka kamili ya kujiongoza. 1972, Mizoram ilikuwa sehemu ya Assam.

Kiini cha mgogoro huo ni madai ya Mizoram dhidi ya sehemu ya ardhi, ambalo jimbo hilo linadai inamilikiwa na wananchi wake kwa zaidi ya miaka 100, huku Assam wakituhumu jimbo hilo kupora kwa nguvu ardhi hiyo.

error: Content is protected !!