January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi ifanyie kazi tamko la THBUB- Lipumba

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahm Lipumba akizungumzia barua kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amelitaka Jeshi la Polisi kuyafanyia kazi matamko yaliyotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Matamko ya THBUB yalitokana na uchunguzi walioufanya dhidi ya tukio la Januari 27 mwaka huu, ambapo jeshi hilo liliwapiga na kuwakamata wafuasi wa CUF waliokuwa kwenye mkutano, maeneo ya Mtoni Mtongani jijini Dar.

Kwa mujibu wa THBUB, walibaini kuwa, jeshi lilitumia nguvu kupita kiasi na kusababisha majeraha kwa baadhi ya wananchi, na hivyo kukiuka misingi ya utawala bora na hawakuheshimu haki za binadamu.

Pia, kulikua na udhalilishaji dhidi ya wanachama wawili wanawake wa CUF, ambao walikamatwa na kuwapelekwa mahabusu. Pia jeshi linadaiwa kutokuzingatia uhuru wa vyombo vya habari ambapo waandishi waliunganishwa na wafuasi wa CUF kupelekwa kituoni.

THBUB ilitoa tamlo lake baada ya uchunguzi na kushauri jeshi lizingatie sheria na haki za binadamu, litoe mafunzo kwa maafisa wa polisi, lizingatie uhuru wa vyombo vya habari na kupatiwa mafunzo yahusuyo misingi ya utawala bora.

Hivyo, kutokana na uchunguzi huo, Mwenyekiti wa THBUB Bahame Nyanduga, amechukuwa jukumu la kumwandikia barua Prof. Lipumba, ikionesha udhaifu wote uliofanywa na jeshi la polisi.

Akizungumzia barua hiyo leo, Prof. Lipumba amesema, “Naipongeza sana THBUB kwa uchunguzi wao, kwani wametenda haki, maana kila mtu aliona yaliyojiri siku ile kwa hiyo majibu yalikuwa wazi, japo kesi bado haijaisha, na tarehe 4 mwezi huu, tunaenda tena mahakamani”.

Ameongeza, “Serikali yetu inafanya madudu na kila madudu yao sasa yamewekwa wazi na serikali yenyewe. Maana uchunguzi huu ungekuwa umefaywa na watu wengine wasingeamini. Sasa basi niwatake tu wayafuate maagizo yaliyotolewa”.

error: Content is protected !!