January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi: Haitakibeba chama chochote cha siasa

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limesema halipo tayari kukipendelea chama chochote kile cha siasa katika kipindi hiki cha uchaguzi utakaofanya Oktoba 25 mwaka huu. Anaadika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi, Charles Mkumbo, wakati akizungumza na wanahabari.

Mkumbo amesema kuwa katika kipindi hiki, jeshi halitakuwa tayari kukipendelea chama cha siasa kwani lipo kwa ajili ya kutenda haki na kulinda raia.

Amesema kuwa wananchi wamekuwa na dhana na imani potofu ya kwamba Polisi hupendelea baadhi ya vyama vya siasa, ambavyo ndivyo sivyo na kwamba Wananchi wanapaswa kuwa na imani na Jeshi hilo.

“Tutafanya kazi kwa kufuata sheria na pale tutakapo ona uvunjifu wa amani unatoweka hatusita kuongeza nguvu ya Polisi.

“Kama ulivyoniuliza kwamba kuna upendeleo wa chama tawala, kitu hicho hakitakuwepo sasa hivi, hata juzi pale Nyegezi wafuasi wa Chadema na CCM walitaka kuleta fujo tulifika na kudhibiti,” amesema Mkumbo.

Sanjali na hayo pia Mkumbo aliyaonya makundi ya watu yatakayofanya fujo siku ya uchaguzi kuacha Mara moja kwani hayatafumbiwa macho, yatachukuliwa hatua za kisheria.

Mkumbo amesema kuna vikundi vichache vilivyoandaliwa na baadhi ya vyama vya siasa ili kuwafanyia fujo wazee na wanawake siku ya uchaguzi na kwamba wanaendelea kufanya uchunguzi ili kuyadhibiti mapema.

error: Content is protected !!