May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Dar yawashikilia 40, wanne tuhuma za mauaji

Kamanda Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo

Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania, linawashikilia watu 40 kwa makossa mbalimbali ya unyan’ganyi wa kutumia nguvu wakiwemo wanne kwa tuhuma za mauaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Watuhumiwa hao wanne, wanatuhumiwa kumuua dereva wa bodaboda Jumanne Mohamed Mussa (30), eneo la Tundwi Songani,
wilaya ya Kigamboni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, tarehe 16 Julai 2020, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema, watuhumiwa hao wanne ni; Malikia Luhende (42), Mfugaji, Mkazi wa Tundwi Kigamboni na wenzake watatu.

Amesema, mtuhumiwa huyo na wenzake watatu, tarehe 03 Julai 2021, walikula njama na wakamuua dereva bodaboda huyo kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani na kumtelekeza vichakani na pikipiki yake.

Kamanda Muliro amesema, upelelezi wa kisayansi ulifanyika na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao na baadhi ya vielelezo na walipohojiwa walikiri kutekeleza mauaji hayo, watuhumiwa watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Kuhusu watuhumiwa wengine 40, Kamanda Muliro amesema, wanatuhumiwa kwa makosa ya unyan’ganyi wa kutumia nguvu, uvunjaji na uporaji wa mikoba ya kinamama kwa kutumia pikipiki @ vishandu.

Amesema, watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia oparesheni ya kuanzia tarehe 01 hadi 15 Julai 2021 na walikamatwa wakiwa na vielelezo mbalimbali.

Amevitaja baadhi ya vilelezo hivyo ni; magari matatu ambayo ni T 820 BED Suzuki carry, T838 ALY Toyota Mark II yaliyokuwa yanatumika kubebea mali za wizi na gari T 396 BVR Toyota Double Cabin iliyokuwa imebeba vyuma viliyoibwa huko Kigamboni Kisarawe II katika mradi wa Serikali wa tenki la maji.

Pia, wamekamatwa na pikipiki sita za aina mbalimbali zilizokuwa zinatumiwa na waporaji wa mikoba na mabegi.

“Televisheni nane za aina mbalimbali, laptop moja zilizoibwa katika matukio ya uvunjaji nyakati za usiku maeneo ya pembezoni mwa Jiji,ambazo zilikutwa kwa wahalifu.”

“Bastola bandia (toi) moja ambayo utumiwa na wahalifu wa matukio ya uvunjaji usiku na unyang’anyi wa kutumia nguvu kutishia watu na kufanikiwa kufanya uporaji,” amesema Kamanda Muliro.

error: Content is protected !!