Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi Dar yawakamata 161 tuhuma wizi magari, pikipiki
Habari Mchanganyiko

Polisi Dar yawakamata 161 tuhuma wizi magari, pikipiki

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Dar es Salaam
Spread the love

 

JESHI la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, nchini Tanzania, limewakamata watu 161 kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo za wizi wa magari, vifaa vya magari na pikipiki. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Alhamisi, tarehe 6 Mei 2021 na Kanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini humo.

Amesema, tarehe 26 Aprili hadi 2 Mei 2021, Polisi kanda hiyo, liliendelea na oparesheni maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kukamata watuhumiwa 161.

“Katika idadi ya watuhumiwa hao 161, watuhumiwa watano vinara wa wizi wa pikipiki, wamekamatiwa Zanzibar wakiwa na pikipiki 40 za wizi.”

“Watuhumiwa hawa wamekuwa wakiiba pikipiki hapa jijini Dar es Salaam, Morogoro na Pwani na kuzipeleka Zanzibar kutafuta wateja,” amesema Mambosasa.

Amesema, watuhumiwa hao wataletwa Dar es Salaam kutoka Zanzibar pamoja na vielelezo na watafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria.

Aidha, katika oparesheni hiyo, Kamanda Mambosasa amesema, “tulifanikiwa kukamata magari mawili aina ya Toyota Noah lenye namba T 770 ACY na Toyota IST yenye namba T 137 DMM magari haya yote yaliibiwa Aprili na kupatikana Mei 2021.”

Amesema, vilevile walikamata silaha ndogo bastola aina ya BROWNING COURT yenye namba B113558 TZ CAR 110526 ambayo iliibiwa tarehe 7 Aprili 2021, maeneo Chanika Lubakaya nyumbani kwa mtoa taarifa, ambapo kikosi kazi cha Jeshi la Polisi kilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kuikamata silaha hiyo tarehe 01 Mei 2021, maeneo hayohayo ya chanika.

Kamanda huyo wa polisi amesema, katika oparesheni hiyo, walifanikiwa kukamata vitu mbalimbali vidhaniwavyo kuwa ni vya wizi kama kama vile; pikipiki 91, TV za aina mbalimbali, ving’amuzi vyake, Subwoofer na Computer .

Pia, walikamata, pikipiki za matairi matatu (Bajaji) nne, Bello 24 za nguo za mitumba, vifaa vya umeme, simu za mkononi, mitungi ya gesi na vipuri vya magari kama vile milango ya magari, taa za magari, mabampa ya magari, Power window na Gia box.

“Oparesheni hii ni endelevu, itaendelea kufanyika ili kuhakikisha jiji letu linaendelea kuwa shwari,” amesema Mambosasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!