December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Dar yavuruga Bawacha

Spread the love

JESHI la Polisi limevamia na kuvuruga maandamano ya amani ambayo yaliandaliwa na Baraza la wanawake Chadema (BAWACHA), licha ya kupewa taarifa siku tatu kabla juu ya kufanyika kwa mkutano huo. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Aidha, mkutano huo uliovurugwa ulitakiwa uanzie maeneo ya Mlimani city Mwenge hadi Uwanja wa Tanganyika Packers Kawe ambapo Mke wa Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa alitakiwa kuongea na wanawake wote wa Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo la uvamizi, Katibu Mkuu wa Bawacha Grace Tendega amesema wamesikitishwa na tukio hilo kwani uongozi wa Chama hicho ulitoa taarifa mapema na kwamba walishaulipia uwanja huo.

Tendega anasema, lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuwasha mishumaa ya amani wakiongozwa na Mama Lowassa ambapo alipanga kuzungumza na kinamama juu ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kwani yakitokea machafuko kinamama ndio waathirika wakuu.

‘Kisheria barua inatakiwa kujibiwa ndani ya masaa 24 lakini cha ajabu hatukujibiwa ndani ya siku tatu baada ya sisi kuanza maandamano ndo ametuletea barua ya kuzuia maandamano yetu licha ya kujitetea kuwa maandamano yetu yalikuwa ya amani’.

Amesema, barua waliyoipokea leo kutoka Makao makuu ya Polisi iliwakataza kufanya maandamano wala mkutano wowote kwa kile alichodai kuwa njia walizokuwa wamepanga kupita wangesababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

error: Content is protected !!